Tuesday, September 03, 2013

MISS TANZANIA 2012 BRIGITTE ALFRED AONDOKA KWENDA KAMBI YA MISS WORLD INDONESIA


Mwakilishi wa Tanzania katika mashindano ya Urembo ya Dunia, Miss Tanzania 2012, Brigitte Alfred Lymo, ameondoka nchini jana kwenda nchini Indosia katika kambi ya Miss World 2013. Pichani juu ni Brigitte akiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam jioni hii tayari kwa safari hiyo.

Akiongea na waandishi wa habari muda mfupi kabla ya kuondoka nchini akiwa uwanjani hapo Brigitte ameahidi kufanya vyema katika mashindano hayo huku akiwaomba watanzania kumpa suport kwa kumpigia kura pindi zoezi hilo liytakapo anza kupitia tovuti ya Miss World.
 Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania, kupitia kampuni ya Lino International Agency, Hashim Lundenga akimwelekeza machache mrembo huyo kabla ya kuondoka.
 Lundenga akizungumza huku Miss Tanzania 2013, Brigitte Alfed na mama yake wakisikiliza.
 Baadhi ya viongozi wa Kamati ya Miss Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na mrembo huyo uwanja wa Ndege jana
  Baadhi ya viongozi wa Kamati ya Miss Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na mrembo huyo uwanja wa Ndege jana
Mama na Mwana....Miss Tanzania akilamba picha na mama yake kabla ya kuruka kwenda Indonesia jana.SOURCE: FATHER KIDEVU BLOG

No comments:

NAIBU WAZIRI WA FEDHA AMWAKILISHA WAZIRI WA FEDHA KATIKA KONGAMANO LA 16 LA MWAKA LA WATAALAM WA UNUNUZI NA UGAVI – ARUSHA

Naibu Waziri wa Fedha, Mheshimiwa Mhandisi Mshamu Ali Munde, amemwakilisha Waziri wa Fedha katika ufunguzi wa Kongamano la 16 la Mwaka la Wa...