KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA, JOHN CASMIR MINJA AHUDHURIA MAADHIMISHO YA SIKU YA MAGEREZA NCHINI ZAMBIA
Askari wa Magereza wa Zambia wakipita mbele ya Mgeni Rasmi, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Zambia, Mhe. Edgar Lungu(hayupo pichani) katika Mwendo wa haraka kama wanavyoonekana Kikakamavu wakati wa Maadhimisho ya Magereza Day ya Zambia ambapo Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Tanzania, John Casmir Minja hivi karibuni alihudhuria Maadhimisho ya Siku ya Magereza huko Kabwe, Zambia.
Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Tanzania, John Casmir Minja(wa tatu kulia) akiwa amesimama katika Jukwaa Kuu kupokea heshima wakati Gwaride la Askari wa Magereza wa Zambia likipita mbele ya Mgeni Rasmi katika Maadhimisho ya Siku ya Magereza nchini Zambia Septemba 26, 2013 (wa kwanza kushoto), Waziri wa Mambo ya Ndani wa Zambia(Mb) Mhe. Edgar Lungu. Wengine ni Mkurugenzi wa Magereza anayesimamia Uzalishaji na Urekebishaji katika Taifa la Sudani Kusini(wa kwanza kulia) akiwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Magereza.
Mkuu wa Jeshi la Magereza Zambia, Kamishna wa Magereza Percy Chato(wa kwanza mstari wa kwanza) akiwa na Kamishna Jenerali wa Magereza Tanzania, John Casmir Minja(wa kwanza mstari wa pili) wakiangalia Gwaride Maalum la Maadhimisho ya Siku ya Magereza nchini Zambia. Maadhimisho hayo yamefanyika hivi karibuni Septemba 26, 2013 katika Chuo cha Mafunzo ya Maafisa Magereza, Kabwe Zambia.
Mkuu wa Jeshi la Magereza Zambia, Kamishna wa Magereza Percy Kato( wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Kamishna Jenerali wa Magereza Tanzania, John Casmir Minja(wa tatu kulia) alipotembelea Ofisi za Makao Makuu ya Jeshi la Magereza Zambia kufuatia Mwaliko rasmi wa Sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Magereza Zambia
Mgeni Rasmi katika Maadhimisho ya Siku ya Magereza Nchini Zambia, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Zambia, Mhe. Edgar Lungu (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi mbalimbali wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama wa Zambia pamoja na Viongozi Waandamizi wa Serikali(wa tatu kulia) ni Kamishna Jenerali wa Magereza Tanzania, John Casmir Minja.Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza
Comments