Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Bi, Beatrice Singano Mallya akiongea kuhusu
kuboreshwa kwa huduma mpya ya Airtel
Yatosha inayomwezesha mteja wa Airtel kupata kifurushi cha maongezi, sms na
internet na kuwasiliana na mitandao yoyote nchini, sasa kwa shilingi 499 mteja
anapata dakika 20, sms 300 pamoja na kifurushi cha internet cha 125 MB.
* Wateja
wa Airtel waongezewa dakika za maongezi, SMS na Interneti zaidi katika
vifurushi vya Airtel Yatosha
* Kwa
shilingi 499 mteja anapata dakika 20, sms 300 pamoja na kifurushi cha internet
cha…

cha 125MB
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imetangaza
kuboresha vifurushi vyake vya huduma ya Airtel Yatosha hivyo kuvifanya kuwa
bora, vya ushindani na gharama nafuu
nchini.
Akiongea kuhusu kuboreshwa kwa huduma hiyo, Mkurugenzi
wa mawasiliano wa Airtel Bi, Beatrice Singano Mallya alisema "huduma ya Airtel Yatosha
inaendelea kutosha kuliko yoyote nchini! sasa vifurushi vya Airtel Yatosha vya
siku vimeendelea kuboreshwa na kuwa vya gharama nafuu zaidi, kwa shilingi 499
mteja anapata dakika 20, sms 300 pamoja na kifurushi cha internet cha 125MB.
Bei ni poa na ya gharama nafuu ukilinganisha na huduma nyingine za vifurushi
zinazotelewa sokoni"
Bi. Singano alisema sambamba na hili vifurushi vya
Airtel Yatosha vinamuwezesha mteja kupiga simu kwenda mtandao wowote ule nchini
wakati wowote masaa 25 yaani mteja anafaidika na vifurushi hivi kwa masaa 24 na
1 la nyongeza siku saba za wiki
Kikubwa na kizuri zaidi mteja anapojiunga na vifurushi
hivi anapata nafasi ya kuingia kwenye promosheni yetu kabambe ya Airtel Yatosha
Shinda Nyumba na kujishindia pesa taslimu au nyumba za kisasa zilizoko Kigamboni jijini Dar es
saalam"
"Airtel inaendelea na dhamira yake ya kuboresha
huduma zake ikiwemo Airtel money yatosha pamoja na vifurushi vya Airtel yatosha
vilivyo na gharama nafuu na kukuwezesha kuwasiliana kwa gharama nafuu zaidi
ndani na nje ya nchi". aliongeza mmbando
Kujiunga na vifurushi mbalimbali vya Airtel yatosha
mteja anatakiwa kupiga *149*99# na kuchagua kifurushi kinachokithi mahitaji
yake. Airtel yatosha inapatikana katika
vifurushi vya siku, wiki au mwezi na vifurushi vyake vinadumu kwa masaa
25 kwa siku.
Comments