Mshindi wa taji la Redd’s Miss Tanzania Top Model 2013, Narietha Boniface akipozi kwa picha mara baada ya kushinda taji hilo jana na kuwa mrembo wa pili kuingia katika nusu fainali za Miss Tanania 2013 baada ya kuwashinda warembo wenzake 29. Shindano la Miss Tanzania Top Mode lilifanyika katika Hoteli ya Snow View Arusha na kuwashirikisha warembo 30.
Mshindi wa taji la Redd’s Miss Tanzania Top Model 2013, Narietha Boniface (katikati) akipozi kwa picha na mshindi wa pili Elizabeth Pert (wapili kushoto), mshindi wa tatu Svetlana Nyameyo (wapili kulia), mshindi wan ne Happiness Watimanywa ambaye pia ni Miss Tanzania Photogenic 2013 na Mshindo wa tano Latifa Mohamed, mara baada ya kushinda taji hilo jana ambapo Narietha amekuwa mrembo wa pili kuingia katika nusu fainali za Miss Tanania 2013 baada ya Miss Photogenic. Shindano la Miss Tanzania Top Mode lilifanyika katika Hoteli ya Snow View Arusha na kuwashirikisha warembo 30.
Warembo walipo jinadi kwa pozi kali na miondoko ya kufa mtu katika kuwania taji hilo la Redd's Miss Tanzania Top Model 2013 ndani ya Snow View Hotel Arusha.
Wadau kutoka TAN MEDIA ambao ni waendeshaji wa Radio Gwala (Radio 5) ya jijini Arusha wakifuatilia kwa ukaribu shindano hilo wakiongozwa na Fransic
Emma Mroso kutoka JAZZ Collection ya jijini Arusha akipozi na warembo waliovaa mavazi kutoka kampuni hiyo.
Wadau mbalimbali wakifuatilia shindano hilo.Picha Zote na Mroki Mroki
Comments