Japan: Samaki wliotoka kwetu ni salama hawajaathirika na mionzi



TAARIFA KWAWAANDISHI WA HABARI
SAMAKI AINA YA MACKEREL WALIOINGIZWA NCHINI TOKA
JAPAN
Hivi karibuni kumekuwa na taarifa katika vyombo vya habari kuhusiana na
samaki aina ya mackerel ambao wanadhaniwa kuwa na mionzi hatari ya
nuklia. Ubalozi wa Japan unapenda kutoa taarifa ifuatayo kuthibitisha ukaguzi
wa samaki kuhusiana na mionzi kabla ya kusafirishwa nje ya nchi.
Baada ya tukio la tetemeko la ardhi lililotokea tarehe 11 Machi, 2011, Wizara
ya Afya, Kazi na Ustawi wa Jamii pamoja na Wizara ya Kilimo, Misitu na
Uvuvi za Japan zimekuwa zikifanya ukaguzi wa mara kwa mara wa maji na
chakula ili kubaini kama kuna dalili za mionzi hatari . Mamlaka hizi
zimekuwa zikifanya uchunguzi kuangalia kama mazao ya baharini pamoja na
hao samaki wa mackerel wanaweza kuwa wameathiriwa na mionzi hatari
iliyotokana na kinu cha nuklia cha Fukushima ambacho kiliathirika na
tetemeko la ardhi. Katika uchunguzi huo hapajaonekana athari zozote katika
mazao ya baharini hususani samaki aina ya mackerel .
Endapo samaki hawa wange vuliwa kabla ya tarehe 11 Machi 2011, hakuna
uwezekano kuwa samaki hao wataathirika na mionzi ya nuklia.
Shirika la Uvuvi la Japan chini ya Wizara ya Kilimo, Misitu na Uvuvi ya
Japan limewasiliana na na kampuni ya Kaneyama Corporation ambayo ndiyo
ilisafirisha hao samaki kuja Tanzania na wamethibitisha kwa nyaraka toka
shirika la Japan Frozen Inspection Corporation kwamba tani 124.992 za
samaki waliosafirishwa kuja nchini Tanzania hazina aina yoyote ya mionzi
hatari kwa binadamu (angalia kiambatanisho). Mbali na hilo samaki hao
walivuliwa katika mwambao wa Choshi, Chiba Prefecture tarehe 16-17
Desemba 2010 na kusafirishwa hadi bandari ya Hasaki iliyopo Ibaraki
Prefecture mnamo tarehe 17 Desemba, 2010. Kwa msingi huo samaki
hawakuathirika na mionzi ya nuklia.
Tunapenda kuhitimisha kuwa hawa samaki wa mackerel kutoka Japan
wamezoeleka hapa nchini Tanzania kutokana na urahisi wa kupatikana
pamoja na matumizi mazuri. Pia wamekuwa chanzo cha protini kwa walaji,
hivyo ni imani yetu kuwa ulaji wa samaki hawa utaendelea. Japan ina imani
pia kuwa Tanzania ni nchi mojawapo kati ya nchi ambazo zinanunua bidhaa
za chakula kutoka Japan na hatua zaidi zinachukuliwa kuongeza ushirikiano
kati ya nchi zetu mbili.
Mwisho wa taarifa.
Waandishi wakiwa na maswali, tuma haya yafikie
embassyofjapan_TZ@dr.mofa.go.jp

Comments