Sunday, August 14, 2011

Mafuta bei juu tena

Meneja wa Biashara wa Mamlaka ya udhibiti wa nishati na maji(EWURA)Mhandisi Godwin Samweli akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo,alipotangaza bei mpya ya mafuta,kulia ni Mkuu wa Idara ya Mawasaliano na Uhusiano Titus Kaguo. Picha na Michael Jamson

&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&

Kama ilivyo ada, na kulingana na Kanuni ya Kukokotoa bei za
bidhaa za mafuta ya petroli bei zimekuwa zikikokotolewa na kutangazwa na
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kila baada ya wiki mbili.
EWURA inatangaza bei elekezi/kikomo za mafuta ya petroli nchini zitakazoanza kutumika
kuanzia Jumatatu, Tarehe 15 Agosti 2011.
Bei hizi zimekokotolewa kwa kuzingatia kanuni mpya

iliyoanza kutumika mwanzoni mwa mwezi huu. Pamoja na kutambua bei elekezi/kikomo za bidhaa
mbalimbali za petroli nchi nzima, ni muhimu kuzingatia yafuatayo:

(a) Bei za jumla na rejareja kwa aina zote za mafuta zimepanda ikilinganishwa na bei zilizokokotolewa kwa ajili ya kuanza kutumika tarehe 1 Agosti 2011 ambazo zilitangazwa tarehe 3 Agosti 2011. Katika toleo hili bei zimepanda kama ifuatavyo: Petroli TZS 100.34 sawa na asilimia 5.51, Dizeli TZS 120.47, sawa na asilimia 6.30 na Mafuta ya taa TZS 100.87, sawa na asilimia 5.30. Mabadiliko haya ya bei za mafuta nchini yametokana na kupanda sana kwa bei ya mafuta katika soko la dunia na kuendelea kushuka kwa thamani ya Shilingi ya Tanzania ikilinganishwa na dola ya Marekani (sarafu ambayo hutumika katika manunuzi ya bidhaa za mafuta kwenye soko la dunia).

Kwa mfano, kwa viwango vya bei zilizotumika katika chapisho hili, bei katika soko la dunia zimepanda kwa wastani wa asilimia 5.42 na thamani ya shillingi ya Tanzania imeshuka kwa shilingi 47.12 (asilimia 2.96) kwa dola moja ya Marekani. Bei za jumla kwa kulinganisha matoleo haya mawili zimepanda kama ifuatavyo: Petroli TZS 110.34 sawa na asilimia 5.70; Dizeli TZS 120.47 sawa na asilimia 6.54; na Mafuta ya Taa TZS 100.87 sawa na asilimia 5.49.

(b) Bei za rejareja na za jumla zingepanda zaidi endapo formula ya zamani ingeendelea kutumika. Kwa kulinganisha vigezo vilivyo katika fomula ya zamani na fomula mpya, bei za mafuta zingekuwa kama ifuatavyo: SOURCE: EWURA

No comments: