Friday, August 05, 2011

Azam FC ziarani Uganda & Rwanda

Mshambuliaji wa timu ya Azam Mrisho Ngassa (juu) kifungia timu yake bao la tatu kwa tikitaka wakati wa mechi ya kirafiki dhidi ya JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Azam uliopo Chamazi nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam jana Azam ilishinda bao 3-2, Picha na Jackson Odoyo


&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&

Mshambuliaji wa timu ya Azam Mrisho Ngassa kifungia timu yake bao la tatu kwa tikitaka wakati wa mechi ya kirafiki dhidi ya JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Azam uliopo Chamazi nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam jana Azam ilishinda bao 3-2,Picha na Jackson Odoyo
BAADA ya kumalizia mechi za kilafiki na timu za hapa nyumbani hapo kesho jumamosi tarehe 6/8/2011, ambapo itacheza na Polisi Dodoma kwenye uwanja wa Azam Stadium, Azam FC inatarajiwa kuondoka siku ya Jumatatu machana na shirika la ndege la (Uganda Air Uganda) kuelekea nchini Uganda na Rwanda kukamilisha ziara yake ya maandalizi ya ligi kuu VPL inayotarajiwa kuanza August 20 mwaka huu.
Azam FC wataondoka kuelekea Uganda August 8 mwaka huu, wakiwa huko watacheza mechi nne za kujipima dhidi ya timu zinazoongoza katika ligi kuu ya Uganda.
Kikosi kamili cha Azam kitawasili nchini jijini Kampala, Uganda siku hiyo hiyo na kucheza mchezo wake wa kwanza August 9 dhidi ya mabingwa wa ligi ya Uganda Bunamwanya FC mchezo utakaochezwa katika uwanja wa Nakivubo.
Baada ya mechi hiyo siku inayofata timu itakuwa mapumziko na kufanya ziara katika ofisi za ubalozi wa Tanzania nchi Uganda ‘Tanzania High Commission’.
Siku ya Alhamis ya tarehe 11 August, Azam FC watacheza dhidi ya Sport Club Villa ya nchini humu na siku ya Ijumaa itacheza na KCC FC mechi zote zitachezwa katika uwanja wa Nakivubo.
Timu itapumzika siku moja kabla ya kucheza na Victors FC ambao ndiyo wenyeji wa Azam FC nchini Unganda siku ya Jumamosi ya tarehe 14 August, huo utakuwa mchezo wao wa mwisho kukamilisha ziara ya nchini Uganda, Azam FC itapumzika siku inaofata kwa maandalizi ya kuelekea nchini Rwanda siku ya Jumanne tarehe 16/08/2011 na kucheza na Polisi Rwanda siku inayofuata tarehe 17/08/2011. Azam FC watarejea Tanzania tarehe 18/08/2011 tayari kuanza ligi kuu ya Vodacom.
Baada ya kukamilika ziara hiyo timu itarejea katika mazoezi ya siku mbili kwa ajili ya mechi ya yake ya kwanza ya ligi kuu ya Vodacom VPL, dhidi ya Moro United itakayofanyika Azam Stadium jijini Dar es Salaam.

No comments: