Profesa Haroub Othman afariki dunia



MHADHIRI mwandamizi wa Chuo Kikuu Cha Dar-es-Salaam, Professa Haroub Miraji Othman, 66, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika Hoteli ya Abuso Shangani Mjini Zanzibar.

Kwa mujibu wa Msemaji wa familia hiyo, Ali Uki alisema kifo cha Professa kilitokea ghafla akiwa usingizini wakati mke wake akimuamsha na kuona haamki ndipo alipowaita watu kumsaidia ambapo aliomba msaada wa kuitiwa daktari kuja kumpima na kuthibitisha kwamba ameshafariki majira dunia majira ya 1:30 asubuhi.

Professa Othman alifika Zanzibar juzi asubuhi akitokea Dar es Salaam kwa ajili ya kuhudhuria uzinduzi wa kilichotungwa na Professa Thomas Burgess, Ali Sultan Issa na Maalim Seif Sharif Hamad kiitwacho ‘Race Revolution and the Struggle for Human Rights in Zanzibar katika hafla iliyofanyika katika ukumbi mpya wa Al- Yamin Funguni Mjini hapa na baadae kuhudhuria uzinduzi wa Tamasha la Nchi za Jahazi (ZIFF) hadi usiku wa saa sita ambapo baadae alikwenda katika hoteli ya Abuso iliyopo Mji Mkongwe akiwa na mkewe Professa Said Othman..

“Professa hakuumwa jana si mlimuona alivyokuwa katika usinduzi wa kitabu asubuhi na usiku alikuwa katika uzinduzi wa tamasha la ZIFF na amefariki alfajiri kwa hakika kila mtu yatamfika mauti yeye ametangulia na sisi tupo nyuma yake ndio ameshatutoka tunachofanya sasa ni kuwasiliana na jamaa kwa ajili ya matayarisho ya mazishi,” alisema msemaji huyo.

Comments

Dah! Prof. Haroub Othman alinifundisha pale Mlimani. Alikuwa mmoja kati ya maprofesa wazuri kabisa na wachambuzi makini wa masuala ya kisiasa na maendeleo na alijulikana Afrika na ulimwenguni kote. Tanzania imempoteza Msomi makini na hili ni pengo kubwa sana. Mungu ampe pumziko jema!
Anonymous said…
Thе post has еѕtablіshed uѕeful to mysеlf.
It’s ехtгemely helpful and you're simply naturally extremely knowledgeable in this field. You get opened up our eye in order to numerous thoughts about this kind of subject together with intriquing, notable and strong written content.

Here is my web blog Buy CIALIS Online
My weblog ... Buy CIALIS Online