Wednesday, June 10, 2009

JK amnusuru Waziri Mkulo


Rais Jakaya Kikwete amehutubia taifa kupitia kwa wazee wa Mkoa wa Dodoma na wabunge. Amezungumzia zaidi msukosuko wa uchumi duniani kwa mapana yake na hali ya uchumi kwa ujumla; na overview ya bajeti. Kwa namna fulani, ni kama ame-pri-empty hotuba ya bajeti ya Waziri wa Fedha ya kesho. Ameibua kitu kipya cha serikali kudhamini madeni ili kupunguza makali ya uchumi wa dunia. Mdau kanitumia SMS akihoji, je, hiyo si EPA nyingine? Reuters wameandika hivi na Hotuba Kamili Hii Hapa.

Wakati huo huo, Kurugenzi ya Mwasiliano Ikulu imesema yafuatayo: Mambo makuu katika Hotuba ya Rais, Dodoma, – jumatano, Juni 10, 2009.

1. Rais ameelezea hali ya mtikisiko wa uchumi duniani, chimbuko la mtikisiko huo na athari za hali hiyo kwa uchumi wa Tanzania. Athari hizo ni kama ziafuatazo:

(a) Bei na mahitaji ya bidhaa za Tanzania kwenye masoko ya kimataifa yamepungua.
(b) Mahitaji na bei za madini ya vito vimepungua kwenye masoko ya kimataifa
(c) Mahitaji ya mazao ya kilimo ya Tanzania kama vile maua na mboga yamepungua kwa asilimia 25
(d) Viwanda vya ngozi, nguo, nyuzi na mavazi pia vimeathirika na hivyo kuathiri pia upatikanaji wa ajira nchini
(e) Sekta ya utalii ambayo ndiyo kubwa kwa uingizaji wa fedha za kigeni pia imeathirika kwa watalii wanaokuja nchini kupungua
(f) Mapato ya Serikali pia yamepungua na hivyo kuathiri mapato ya ndani na mapato ya fedha za kigeni
(g) Uwekezaji kutoka nje umepungua pia na baadhi ya makampuni yaliyokuwa yanataka kuja kuwekeza Tanzania, ama yameahirisha ama yamefuta mipango yao ya uwekezaji. Mifano ni mradi wa uwekezaji katika nickel pale Kabanga, Ngara, Kagera na miradi ya umeme, saruji, mbolea na aluminium smelter mkoani Mtwara
(h) Hali ya ajira nchini imekuwa mbaya zaidi kwa sababu ya matatizo hayo ya uchumi na hadi Aprili, mwaka huu, kiasi cha watu 48,000 walikuwa wamepoteza ajira
(i) Vile vile kasi ya kukua kwa uchumi wa Tanzania inakadiriwa kuwa itapungua kutoka kwenye asilimia 7.4 kama ilivyobashiriwa mwaka huu hadi kufikia asilimia 5 hadi 6.

Soma kinagaubaga taarifa hapa au upate habari hizi kwa kina.

No comments: