Michael Jackson afariki dunia.


Mwanamuziki wa mkali wa Pop Duniani Michael Jackson amefariki dunia. Kwa mujibu wa shirika la utangazaji la CNN Michael Jacksom amefariki dunia na alikutwa katika jumba lake la kifahari huko Bel-Air akiwa mahututi, habari za awali zinasema alipata Stroke.
Kwa mujibu wa Polisi na msemaji wa kikosi cha Fire Cap. Steve Ruda alisema kuwa walipokea simu ya 911 toka kwenye jumba la Michael walipokwenda walimkuta akiwa katika hali mbaya na kumpa huduma ya kwanza kabla ya kumhamishia UCLA Medical Centre.

Mamia kwa maelfu ya waandishi walikuwa wamekusanyika nje ya Hospital hiyo ambapo habari za ugonjwa na uvumi wa kufariki Michael Jackson ambaye amekuwa kipenzi cha mashabiki wengi ulimwenguni zilikuwa zimeenea kote kwa kasi ya ajabu.
Michael amefariki akiwa na miaka 50.

Mwezi huu unaokuja Michael alitazamiwa kutangaza kustaafu muziki rasmi kwa show kubwa ambayo ilipangwa kufanyika nchini Uingereza
Mungu aiweke roho ya marehemy mahala pema peponi-Amen.

Comments

Anonymous said…
Yani jamaa alishaanza kugeuka kuwa nyani kweli mungu hapigi kwa fimbo, Yote pesa hio imemuharibu sasa kaomdoka kaacha kila kitu duniani na atasema nini huko akhera?