HASHEEM THABEET AJIUNGA NA MEMPHIS GRIZZLIES


Kama uliwahi kutabiri kwamba siku moja mtanzania Hasheem Thabeet atakuja kuchezea katika ligi ya mpira wa kikapu ya NBA, unayo sababu ya kujidai kwani utabiri wako umetimia jioni hii(saa za New York).

Hasheem Thabeet amechaguliwa kujiunga na timu ya Memphis Grizzlies yenye makao yake makuu huko Memphis katika jimbo la Tennessee nchini Marekani.
Hasheem anakuwa mtanzania wa kwanza kufikia hatua hiyo.

Kama nchi tuna kila sababu ya kufurahia mafanikio yake na kumtakia kila la kheri. Hivi sasa anakuwa,bila shaka, “balozi” wetu katika ulimwengu wa michezo hususani mpira wa kikapu. Kila la kheri Hasheem.Soma kinagaubaga taarifa http://www.blogger.com/">hapa

Comments