Wednesday, June 03, 2009

Mzee Kisumo mwenyekiti mpya wa bodi Vodacom


BODI ya Wakurugenzi ya Vodacom Tanzania, imemteua Peter Kisumo (74) kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni hiyo.

Taarifa iliyotolewa Jijini jana na Kampuni hiyo imeeleza kuwa uteuzi huo ulianza rasmi mwezi Aprili mwaka 2009.

Bw. Kisumo anachukua nafasi ya Bw. Ferdinand Ruhinda aliyemaliza muda wake.

Bw. Kisumo ambaye historia yake ilianzia kwenye Vyama vya Wafanyakazi (Trade Union) aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini katika awamu ya kwanza hadi ya tatu.

Kwa mara ya kwanza, aliteuliwa kuwa Waziri kwenye serikali ya awamu ya kwanza mwaka 1964.

Baadhi ya nyadhifa alizoshika ni Mwenyekiti Mtendaji wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Kiwanda cha nguo cha Urafiki, Kiwanda cha Mbao Tanzania (TWICO) na Tanganyika Planting Company Limited (TPC).

Kwa sasa Bw. Kisumo ni Mwenyekiti Mtendaji wa Agro Vet na pia ni Mkurugenzi wa Chama cha Wakulima Tanzania (TFA) na Commercial Bank Africa.

Bw. Kisumo ana mke na watoto watatu na wajukuu kumi--- alistaafu utumishi wa Umma mwaka 2000.

Imetolewa na: Mwamvita Makamba
Mkuu wa Idara Ya Mawasiliano
Vodacom Tanzania Limited

1 comment:

Unknown said...

view publisher site official source visit this website next page look at this site you could try here