Kwaninini na sisi tusiwalete Wamarekani wajifunze kiswahili


Afisa Mwandamizi wa ubalozi wa Marekani nchini Dr. Tulinabo Mushingi (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na vijana wa vyuo vikuu wanaosomea shahada za kwanza wanaosafiri kesho kwenda Marekani kwa programu ya kufundisha lugha ya kiingereza kwa mataifa ya Afrika. Programu hiyo inagharimiwa na watu wa Marekani, ni programu inayofuzwa kwa kina inayolenga kuongeza usomaji kwa lugha ya kingereza, kuandika, kusoma na kusikiliza maarifa ya wanazuoni wa kiafrika lakini kubwa zaidi ni kuwapa welewa mpana zaidi wa tamaduni za kimarekani pamoja na mila na desturi zao. (picha kwa hisani wa ubalozi wa Marekani)
Sijui sisi kama Tanzania tutalifikia suala hili lini, wenzetu wameona mbali saana programu za namna hii ni zenye kufunza makubwa kutoka kwetu ina maana vijana wetu hapo baadaye watajua Umarekani kwa kina zaidi kuliko utanzania, changamoto kwetu tufanyeje tufikie huku????

Comments