Tuesday, June 02, 2009

Baba wa taifa Guinea Bissau aaga dunia


Luis Cabral ambaye aliiongoza Guinea-Bissau mara baada ya kupata uhuru amefariki dunia akiwa nchini Ureno ambako amekuwa akiishi kama mkimbizi tangu kutimuliwa madarakani mwaka wa 1980.

Bwana Cabral ambaye alichukuwa wadhifa wa urais mnamo mwaka wa 1974 aling’olewa madarakani na Joao Bernardo Vieira ambaye aliuawa mwezi Machi mwaka huu.

Kabla ya kuhamia mjini Lisbon, Ureno, Bwana Cabral alikimbilia Cuba.

Taarifa ya serikali ilisema, “Serikali na wananchi wa Guinea-Bissau wanasikitika kutangaza kifo cha mpendwa Luis Cabral.”

Serikali inatarajiwa kuandaa kikao cha dharura kuandaa siku tatu za maombolezo ya kitaifa.
Habari kutoka BBC.

No comments:

HESLB NA ADAPT IT ZAINGIA MAKUBALIANO RASMI

Dar es Salaam, Jumatatu, Disemba 08, 2025 Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imeingia katika hatua nyingine ya mageuzi ya k...