Friday, June 19, 2009

Eti Ze Utamu amekamatwa

Taarifa za awali zilizokuwa zikieleza kuwa Polisi wa Tanzania kwa kushirikiana na Polisi wa Kimataifa (Interpol), kwamba eti walifanikiwa kumshika Raia mmoja wa Uingereza ambaye ana asili ya Tanzania mwenye umri wa miaka 39 na kutuhumiwa kwa kuundesha mtandao wa Ze Utamu.
Raia huyo ambaye alidaiwa kuwa ni Mtaalamu wa kompyuta na ana uwezo wa kuzungumza na kuandika Kiingereza, kiswahili na kichina ana makazi katika mji wa Essex nchini Uingereza.Wataalamu wa Idara ya upelelezi kutoka Tanzania wakishirikiana na wenzao wa Uingereza wamefanikiwa kuonana na mtaalamu huyo na kupata ushahidi kwamba ndiye alikuwa mmiliki wa Mtandao huo. Taarifa za sasa kutoka chanzo cha habari hizo cha, Swahili Time zinaonyesha kuwa chanzo hicho kimelazimika kuiondoa mtandaoni baada ya kuwepo taarifa za kutatanisha, kuhusu ukweli wake. tutaendelea kufahamishana yanayojiri.
Taarifa zaidi zinazosambaa sasa zinaeleza kuwa huyo bwana hajakamatwa. Mmoja aliandika hivi kwenye Bidii: So far ni uzushi.dogo ni mtoto wa mweshimiwa Lusinde,ukoo wa malechela. todate yupo Uk yeye na familia yake wakila kuku raha mustarehe.so all of this news about him ni huzushi. nimeonana na kuongea na wana familia yake wamenithibitishia hilo.Tanzania wanaitaji sana kuinvest kwenye CYBE CRIME TECHNOLOGIES kuliko chochote kile wamaitafuta utamu baada ya Mweshuimiwa Rais kutolewa how about walala hoi waliojiua kutokana na UTAMU?.how about wizi wa mabenki kupitia internet ambao sofar umesababisha zaidi ya 25 million USD kuibiwa katika kipindi cha miezi 7 iliyopita?serikali yetu inakumbatia siasa kuliko technology.wao todate wanaamini watanzania ni mamuma but sio kweli CCM wanatakiwa kujua kuwa Karne ya kupigiwa kura kwa sababu eti wamegawa fulana au pilau zimeisha.kikwete inabidi astafishe vikongwe atoe ajira kwa vijana aone vinginevyo tumeumiaSIKU NJEMA

No comments: