Thursday, June 18, 2009

Shirikisho la Afrika Mashariki la nini sasa kama ni hivi?





Twaelekea katika hilo linaloitwa shirikisho la Afrika Mashariki, kila nchi ina mambo yake lukuki ambayo imeyashindwa au kuelemewa, hawa Wakenya (pichani katika picha zilizopigwa na JOSEPH KANYI) wana mambo yao lukuki yamewashinda wanapigana kila kukicha mpaka inabidi kutumia ulinzi mkali, sisi kule Tarime ni mapanga na mashoka watu wanakatana utadhani sijui ni ng'ombe au kuku, bado huko Uganda kule kwa kina Josseph Kony mambo ni ya hovyo, sasa hivi kuna suala la kisiwa cha Migingo Kenya na Uganda hawapatani, kule Rwanda na Burundi mambo ni haya haya hivi tunataka kuunda shirikiso la aina gani. Zanzibar bado inatusubiri sijui hatima ya watoto wetu?

No comments:

NAIBU WAZIRI WA FEDHA AMWAKILISHA WAZIRI WA FEDHA KATIKA KONGAMANO LA 16 LA MWAKA LA WATAALAM WA UNUNUZI NA UGAVI – ARUSHA

Naibu Waziri wa Fedha, Mheshimiwa Mhandisi Mshamu Ali Munde, amemwakilisha Waziri wa Fedha katika ufunguzi wa Kongamano la 16 la Mwaka la Wa...