Saturday, June 27, 2009

kaimu mufti sheikh Gorogosi afariki dunia


Kaimu Mufti wa Tanzania Sheikh Suleiman Gorogosi amefariki dunia leo mchana baada ya kupata ajali katika kijiji cha Mnolela mkoani Lindi.

Akizungumza na globu hii mkuu wa mkoa wa Lindi Said Meck Sadick amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo majira ya saa saba na robo mchana.

Taarifa zilizopatikana baadaye zinasema kwamba Kaimu mufti ambaye pia ni Sheikh wa mkoa wa Lindi alikuwa anasafiri kutoka katika mji wa Mtwara ambako alishuka na ndege kuelekea Lindi mjini.

Habari zaidi zinasema kwamba bakwata wanaandaa mpango wa maziko ya kiongozi huyo wa bakwata.

No comments:

WAZIRI MKUU MHE. KASSIM MAJALIWA AMALIZA ZIARA YA SIKU MOJA MKOANI MBEYA

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb), leo ameondoka Mkoani Mbeya baada ya kukamilisha zi...