Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, Sheikh Issa Ponda.
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya
Dar es Salaam limemtia mbaroni Katibu wa Jumuiya tajwa hapo juu maarufu
kama PONDA ISSA PONDA kwa makosa mbali mbali ya kuchochea vurugu na
uvunjaji wa amani jijini Dar es Salaam.
Aidha hivi karibuni Sheikh Ponda
Issa Ponda aliongoza kundi la wafuasi wake na kuvamia kiwanja No.
311/3/4 BLOCK “T” eneo la Chang’ombe katika Manispaa ya Temeke mali ya
Kampuni ya AGRITANZA ambayo ipo chini ya Kurugenzi ya Kampuni hiyo.
Mnamo tarehe 12/10/2012 Ponda Issa
Ponda aliwaongoza wafuasi wake walioteka eneo hilo wakidai kwamba
wanakomboa. Mali za Waislamu, zilizouzwa na BAKWATA, uchunguzi wa awali
umeonyesha kwamba kiwanja hicho kina hati miliki No. 93773 uliotolewa na
Wizara ya Ardhi pamoja na mikataba mbali mbali ya kuuziana au
kubadilishana kati ya BAKWATA na Kampuni tajwa hapo juu.
Pia uongozi wa BAKWATA
umeletamashahidi kuthibitisha uhalali wa kiwanja hicho kumilikiwa na
Kampuni tajwa. Hivyo watu wote waliovamia eneo hilo wakiongozwa na
Sheikh Ponda wanakabiliwa na shtaka la kuingia kwa jinai pamoja na
uharibifu wa mali katika eneo hilo.
Sambamba na kukamatwa kwa Sheikh
Ponda tarehe 16/10/2012 saa 4.00 usiku karibu na eneo la maficho yake
ambapo aliletwa na pikipiki.
WATU 38 WAMEKAMATWA KWA KOSA LA KUINGIA KWA
JINAI NA UHARIBIFU
Wakati huo huo sambamba na
kukamatwa kwa Sheikh Ponda Issa Ponda Polisi walifanya operesheni
maalumu ya kuwaondoa wavamizi katika kiwanja tajwa hapo juu
kinachomilikiwa na Kampuni AGRITANZA. Watu wapatao 38 walikutwa katika
eneo la kiwanja hicho ambacho kati ya hao (7) ni wanawake na 31 ni
wanaume.
Operesheni hiyo ilifanyika tarehe
17/10/2012 usiku wa manane kuanzia saa tisa hadi saa kumi na nusu usiku
kwa muda wa dakika 90. Katika eneo hilo vilikutwa vielelzo mbali mbali
vikiwemo visu na mapanga na pia nyenzo mbali mbali za ujenzi, pamoja na
vifaa vya ujenzi, vielelezo hivyo vimehifadhiwa katika kituo cha Polisi
tayari kwa ajili ya ushahidi mahakamani.
SHEIKH PONDA KUSABABISHA VURUGU NA VITISHO
Katika siku za hivi karibuni
Sheikh Ponda Issa Ponda amekuwa akiwaongoza wafuasi wake chini ya
Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania kwa kufanya maandamano kinyume
cha Taratibu na kuhamasisha umwagaji damu jijini Dar es Salaam na nchini
Tanzania kwa ujumla.
Kwa ujumla Jumuiya na Taasisi za
Kiislamu Tanzania inayoongozwa na Sheikh Ponda haijasajiliwa kisheria
lakini wanatihumiwa kwa uchochezi wa hali ya juu ambapo licha ya kufanya
maadamano kinyume na sheria pia siku ya tarehe 12/10/2012 walisababisha
kuvunja kwa makanisa zaidi ya manane, uharibifu wa magari na wizi au
upotevu wa vifaa katika makanisa, yote hayo yameongozwa na Sheikh Ponda
na madhara yake ni makubwa.
Sheikh Ponda amekuwa mstari wa
mbele kupambana na vyombo vya dola pamoja na kuingilia uhuru wa Mahakama
kwa kudai watuhumuwa waliokamatwa kwa uvunjaji wa makanisa na
kufikishwa mahakamani waachiwe mara moja kabla siku saba na kadhalika.
Uchunguzi wa watuhumiwa wote 39
unaendelea na kufikishwa mahakamani mara baada ya kupitishwa na wakili
wa Serikali kuthibitisha mashitaka.S.H. KOVA – DCP
KAMANDA WA POLISI
KANDA MAALUMU YA POLISI
DAR ES SALAAM
1 comment:
Hebu mkuu iweke hii taarifa hapa, ili uone mambo yalivyo, walisema wahenga kila jamblinapotokea, ujue lina sababu:
http://mtayarishaji.blogspot.com/2012/10/ni-kwa-nini-uhalali-kwa-ukabila-udini.html
Post a Comment