Mabanda ambayo watu wamekaa kwa utulivu wakiuaga mwili wa Kamanda Liberatus Barlow.
Umati
mkubwa watu wakiwa katika uwanja wa Nyamagana wakati wa kuuaga mwili wa
aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, SACP Liberatus Barlow.
Afande
George Msangi akiongoza ratiba za kumuaga aliyekuwa Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Mwanza, SACP Liberatus Barlow aliyeuawa usiku wa kuamkia
Jumamosi na watu wanaodhaniwa kuwa majambazi katika eneo la Kitangiri
karibu na hoteli ya Tai Five.
Msafara
wa magari ya kuleta mwili wa marehemu Liberatus Barlow yakiingia katika
uwanja wa Nyamagana ili viongozi na wananchi mbalimbali wapate kuuaga
mwili huo.
Magari yakiingia katika uwanja wa Nyamagana.
Maaskari
walioteuliwa kubeba mwili wa marehemu Liberatus Barlow wakiwa
wamejipanga vyema ili mwili uweze kutolewa ndani ya gari ili uwekwe
sehemu nzuri ambayo kila mtu anaweza kuuaga vizuri.
Hapa wakiushusha kutoka ndani ya gari ili waweze kuubeba.
Safari ya kuelekea sehemu maalum iliyopangwa kwa ajili ya mwili wa marehemu ilianza hivi.
Maaskari wakiwa sawa kutekeleza jukumu lao.
Mkuu
wa Mkoa wa Mwanza, Injinia Everest Ndikillo akielekea kuuaga mwili wa
marehemu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow katika
uwanja wa Nyamagana leo.
Viongozi mbalimbali wa Kiserikali wakisimama kwa dakika chache kuupa heshima mwili wa marehemu Kamanda Liberatus Barlow.
Baadhi ya Maafisa ya Jeshi la Polisi.
Ofisa Usalama wa Taifa, Meja Jacob Mutashi mwenye suti nyeusi kulia akionekana pichani.
Mwili wa Marehemu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow.
Mwandishi Peter Fabian kutoka gazeti la Mtanzania akiweka vizuri picha ya marehemu Kamanda Liberatus Barlow.
Saluti kutoka kwa Maofisa wa Polisi kwa Marehemu Kamanda wa Mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow.
Katibu
wa CCM Mkoa wa Mwanza, Joyce Masunga akiweka saini katika daftari la
maombolezo katika msiba wa marehemu Kamanda Liberatus Barlow katika
uwanja wa Nyamagana.
Mkurugenzi
wa Makosa ya Jinai, Richard Manumba akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya
Magu, Bi. Jackline Wana huku Katibu tawala wa Mkoa wa Mwanza, Bi.
Rosemary Mwanyika akiwa mbele mwenye suti nyeusi.
Ibada
ya kuuaga mwili Marehemu, Kamanda Liberatus Barlow kama ilivyoongoza na
Watumishi wa Kanisa la Roman Catholic maana kamanda alikuwa muumini wa
kanisa hilo.
Wakuu
wa wilaya mbalimbali katika Mkoa wa Mwanza na baadhi ya viongozi wa
serikali, vyama vya kisiasa wakionekana katika picha wakiwa na majonzi
mazito.
Wananchi
mbalimbali kutoka katika Mkoa wa Mwanza na nje ya Mkoa wa Mwanza
wakionekana katika tukio la kuuaga mwili wa Kamanda Liberatus Barlow.
Wanafamilia
wa marehemu, Kamanda Liberatus Barlow wakiwa na majonzi makubwa sana
katika uwanja wa Nyamagana wakati wa kuuaga mwili wa mpendwa wao.
Maafisa
wa Majeshi aina mbalimbali kutoka Tanzania wakionekana katika hafla la
kuuaga mwili wa marehemu, Kamanda Liberatus Barlow.
Mabanda ambayo watu wamekaa kwa utulivu wakiuaga mwili wa Kamanda Liberatus Barlow.
Umati
mkubwa watu wakiwa katika uwanja wa Nyamagana wakati wa kuuaga mwili wa
aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, SACP Liberatus Barlow.
(Picha zote kwa hisani ya B Plus Blog)
No comments:
Post a Comment