Saturday, October 13, 2012

RPC Mwanza auawa kwa Kupigwa Risasi na Majambazi

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow ameuawa kwa kupigwa risasi na majambazi usiku wa kuamkia leo katika maeneo ya Kitangiri jijini Mwanza.

Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Said Mwema amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, na kusema timu ya Makachero kutoka Dar ikiongozwa na Mkurugenzi wa Upepelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba inakwenda jijini humo kuongeza nguvu ya kiupelelezi na taarifa zaidi zitatolewa baadaye.
R.I.P KAMANDA LIBERATUS BARLOW 

No comments:

Ujumbe wa DRC watoa msaada kituo cha wakimbizi NMC - Kigoma

  Waziri wa Nchi, anayeshughulikia  Masuala ya Ustawi wa Jamii, Hatua za Kibinadamu na Mshikamano kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (D...