Waziri
Mkuu mstaafu na mbunge wa Monduli amethibitisha nguvu kubwa ya kisiasa
aliyonayo, baada ya kufanikiwa kushinda kwa kishindo nafasi ya ujumbe wa
NEC wilaya ya Monduli.Lowassa ameshinda kiti hicho kwa kupata kura..
kati ya ..
Dr
Suleshi Toure baada ya kuona hali mbaya kwa upande wake alitangaza
kujitoa, na kusema anamwachia nafasi mgombea mwingine kijana Nanai Taon
Konina aliyepata kura..
Dalili
za Lowassa ambaye wilayani Monduli anajulikana kama Simba, zilionekana
mapema hata kabla ya mkutano, baada ya kuwepo taarifa ya kwamba wana ccm
walipanga kumsindikiza kwa maandamano hadi kwenye ukumbi wa mkutano wa
chuo cha ualimu Monduli.
Akijinadi
mbele ya wapiga kura waliyokuwa wakimshangilia muda wote, Lowassa
alijivunia mafanikio makubwa ambayo wilaya ya Monduli imeyapata katika
sekta ya elimu, afya na barabara, huku uhai wa chama ukiwa mkubwa
tofauti na wilaya nyingine za mkoa wa Arusha.Mkoa wa Arusha ndiyo ngome
kuu ya chama cha upinzani cha CHADEMA.
”Mtu
akiniuliza kwanini nagombea tena nafasi hii ya ujumbe wa NEC, nitamjibu
kwa jeuri kwamba nimefanikiwa kuifanya Monduli kuwa moja ya wilaya bora
nchini”alisema Lowassa na kushangiliwa. Lakini
Dr Toure, alikuwa na wakati mgumu wa kujieleza ambapo alidai kuwa
haridhishwi na kiwango cha maendeleo kilichofikiwa katika wilaya hiyo,
kauli iliyowafanya wajumbe wa mkutano huo mkuu wa wilaya kumzomea.Na
hata alipotangaza kuwa anajitoa, alizomewa.
Mkurugenzi
wa uchaguzi huo Athman Sheshe alisema kuwa kwa mujibu wa taratibu, hata
kama mgombea ametangaza kujitoa lakini jina litapigiwa kura.
Hali
ilikuwa mbaya zaidi kwa mgombea mwengine Nanai Taon Konina, ambapo
alionekana kushindwa kujieleza vizuri, hata alipoulizwa swali na mmoja
wa wpaiga kura kuwa hakuwa mwanachama halali wa CCM bali ni wa CHADEMA
alibabaika na kushindwa kujibu.Msimamizi wa uchaguzi aliingilia kayi
kumsadia kwa kumwambia aombe kura na asijibu swali hilo.
Ushindi
huo wa Lowassa unazidi kudhihirisha mvuto mkubwa aliyonao mwanasiasa
huyo ndani ya CCM.Waziri mkuu mwenziye mstaafu Fredrik Sumaye hapo juzi
alikikwaa kisiki baada ya kushindwa na Dr Mary Nnagu katika nafasi ya
ujumbe wa NEC wilayani Hanang.
No comments:
Post a Comment