Habari
zilizotufikia muda si mrefu ni kwamba kiongozi wa jumuiya ya Uamsho, Ustaadh
Farid amepatikana akiwa katika hali nzuri na kwa sasa yupo kwao kwa mzazi wake
akipumzika. Chanzo; Zanzinews Blog
**********************************************
Amesema kuwa waliomchukuwa walijitambulisha kwake kuwa ni askari polisi na kumonesha vitambulisho huku wengine wawili wakiwa na silaha za mshingani hapo hapo wakamfunga macho yake kwa kutum...ia kitambaa ili asijue wapi anapelekwa walimchukua kwa gari na baadae kumuingiza katika nyumba asioijua kwa mahojiano bila ya kumfungua kitambaa hicho kwa muda ...
wa siku tatu mfululizo.
Amesema kuwa watu hao waliomuhoji maswala mengi sana kuhusu tangu kuuanzishwa kwa jumuia ya uamsho na safari zake za kwenda omani na mpaka kumchukulia simu yake bila ya kumrejeshea pia wametaka kujua kuwa anauhusiano gani na rais shein na makamo wakwanza wa raisi maalim seif, wakati wanamuhoji walifika mpaka kupiga risasi chini ya miguu nyake ili kumtisha na kuweza kufikia lengo lao walilojipangia.
Amesema pia watu waliomchukuwa na baadhi ya waliokuwa wanamlinda hawezi kuwajua kutokana na kuwa walikuwa wamevaa soksi ndani ya nyuso zao nakubakisha macho tu,amsema kutokana tu na lafdhi zao ambazo walikuwa wanaongea inaonekana wazi kuwa wengi ni kutoka bara na wazanzibari ni kama wawili tu kutokana na sauti zao.
kuhusu suala lakupigiwa simu na mtu asiemjua amesena kuwa wao kama viongozi huwa mara nyingi wamekuwa wakipigiwa simu na watu wasiowajua na wamekuwa wakionanan nao bila ya matatizo hivyo basi kitendo cha kupigiwa simu siku hio na mtu asiemjua hakikumshituwwa kwani nikawaida kwao hususani aliemnigia alijitambulisha kama ni mwanafunzi wake wa mahad lmahfudh
Aidha amesema kuwa muda wote huo wa siku tatu hakuweza kula chochote katika chumba hicho kwani alikuwa hawaamini na badala yake alikuwa anakunywa maji kutoka bomba la mfereji lililokuwa chooni katika chumba hicho pia amesema wakati yupo ndani hakujua lolote linaloendelea huku nje isipokuwa amejua baada ya kutoka nje kwa kuambiwa na kila manaemkuta.
Aidha sheikh farid ameiomba serikali ya mapinduzi ya zanzibar kutumuia sheria na uadilifu kwa rai wake kinyume cha hivo watakuwa wanaimba tu katika nchi amani na utulivu usiokuwepo pia amewataka wazanzibar kuendelea kutetea maslahi ya nchi yao kama kawaida kwani kufanya hivo ni haki yao na yeye amewahakikishi ataendelea kuitetea zanzibar mpaka tone la mwisho la damu yae.
SOURE' UAMSHO FACEBOOK
No comments:
Post a Comment