Mwanamuziki kutoka nchini Marekani Rick Ross akiimba jukwaani usiku wa kuamkia leo mbele ya maelfu ya wakazi wa jiji la Dar na vitongoji vyake kwenye viwanja vya Lidaz Club,wakati wa tamasha la Serengeti Fiesta likirindima.
Mwanamuziki kutoka nchini Marekani,Rick Ross akijisikia furahaa kuwaona Watanzania wakiwa wamejitokeza kwa wingi kwa ajili ya kumshuhudia yeye akikamua stejini.
Mkali mwingine wa miduara AT na madansa wake wakilishambulia jukwaa.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka THT,akiimba jukwaani na shabiki wake.
Mashabiki wakitaka kuangusha uzio uliowekwa kwa ajili ya usalama.
Baadhi ya
Askari wakijaribu kuweka usalama wa kutosha kwa Mwanamuziki Rick Ross
imara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Lidaz Club,kwa ajili ya
kutumbuiza kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012.
Viwanja vya Lidaz palikuwa hapatoshi hata kidogo.
Watu kibao wakiwa ndani ya viwanja vya lidaz club usiku wa kuamkia leo
Msanii wa
miondoko ya rusha rohoo a.k.a Miduara,Shilole akijiachia jukwaani
vilivyo na madansa wake usiku wa kuamkia leo mbele ya umati mkubwa
uliofika kwenye viwanja vya Lidaz Club,katika kuhitimisha kilele cha
tamasha la Serengeti Fiesta 2012.
No comments:
Post a Comment