Friday, October 05, 2012

KESI YA ELIZABETH 'LULU' MICHAEL YAGONGA MWAMBA MAHAKAMA YA RUFAA, YARUDISHWA MAHAKAMA YA KISUTU KUANZA UPYA...!!!


KESI ya mauaji inayomkabili msanii wa filamu za maigizo nchini, Elizabeth Michael ‘Lulu’ anayedaiwa kumuua msanii mwenzake, Steven Kanumba ‘The Great’ ambayo leo ilitakiwa kutolewa maamuzi ya umri na Mahakama ya Rufaa imerudishwa mahakama ya Kisutu kuanza upya. 

Akitoa maamuzi hayo Naibu Msajili wa Mahakama hiyo yenye maamuzi ya mwisho hapa nchini, Zahra Marume amesema utaratibu uliotumika kuifikisha kesi hiyo mahakamani hapo ulikuwa na makosa hivyo kuamuru kesi hiyo kurudi mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam.

No comments:

WIZARA YA AFYA YAOMBA SH. TRILIONI 1.8 BAJETI YA 2026/2027

  Wizara ya Afya imeomba kuidhinishiwa jumla ya Shilingi trilioni 1.8 kwa mwaka wa fedha 2026/2027 kwa ajili ya kuendelea kuboresha huduma z...