Wednesday, October 24, 2012

UMOJA WA MATAIFA WATIMIZA MIAKA 67


Waziri wa Afrika Mashariki akishuhudia upandishwaji wa bendera ya Umoja wa Mataifa ikiwa ni ishara ya kusheherekea miaka 67 ya Umoja huo katika viwanja vya Karimjee jijini Dar leo.
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Raphael Muhuga aliyemwakilisha Mkuu wa Majeshi ya Tanzania katika sherehe za maadhimisho ya miaka 67 ya Umoja wa Mataifa tangu kuzaliwa kwake.

Mgeni rasmi Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mh. Samwel Sitta akiwasili katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo katika Kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Umoja wa Mataifa Tanzania kusheherekea miaka 67 tangu uanzishwe.
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dkt. Alberic Kacou akimlaki na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mh. Samwel Sitta kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaa leo.
Pichani Juu na Chini ni Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dkt. Alberic Kacou (katikati) akimtambulisha Mh. Samwel Sitta kwa baadhi ya Wakurugenzi wa Mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa hapa nchini.
Waziri wa Afrika Mashariki Mh. Samuel Sitta akipokea heshima ya wimbo wa Taifa baada ya kuwasili katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo kuhudhuria kilele cha maadhimisho ya wiki ya Umoja wa Mataifa baada ya kutimiza miaka 67 ya UN tangu kuanzishwa.
Mh. Samuel Sitta akikagua gwaride maalum katika kilele cha wiki ya maadhimisho ya Umoja wa Mataifa.
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dkt. Alberic Kacou, Mgeni rasmi Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mh. Samwel Sitta na Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meha Jenerali Raphael Muhuga wakiwa Meza kuu.
Pichani Juu na Chini ni viongozi wa Madhehebu ya Dini nchini wakiomba Dua kwa ajili ya kubariki sherehe za kutimiza miaka 67 ya Umoja wa Mataifa tangu kuanzishwa.
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Samwel Sitta akizungumza katika sherehe za kutimiza miaka 67 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa (UN) katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, Sitta aliipongeza Umoja wa Mataifa kwa kuisaidia Tanzania katika nyanja mbalimbali za maendeleo ili kutokomeza umaskini.Waziri Sitta alisisitiza kwamba bado Umoja wa Mataifa unakabiliwa na changamoto nchini kama vile amani na usalama, tatizo la njaa, mabadiliko ya tabia nchi na uwepo wa silaha za maangamizi.
Katibu wa UNA Tanzania Fancy Nkuhi akizungumza kwenye hafla hiyo alisema umoja wa mataifa imefanya kazi kubwa katika kuwaunganisha vijana wa bara la Afrika. Nkuhi alisema kupitia YUNA walitoa elimu ya afya ya uzazi na ugonjwa wa Ukimwi kwa vijana katika mikoa kumi hapa nchini Tanzania katika harakati ya kuelimisha vijana madhara ya ugonjwa huo na afya ya uzazi kwa vijana.
Wanafunzi kutoka shule ya mchepuo wa kiingereza ya Heritage (Heritage English Medium Schools) ambao walikuwa kivutio wakati wa maadhimisho ya miaka 67 ya wiki ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania wakiwa katika gwaride maalum kupamba sherehe hiyo.
Meza kuu ikifurahia jambo wakati wa gwaride la watoto wa shule ya Heritage baada ya kuonyesha mbwembwe katika kupamba sherehe hiyo.

No comments: