Rafu aliyochezewa Kelvin Yondani na Haruna Moshi 'Boban'.
Mlinzi wa kati wa kutumainiwa wa
klabu ya Young Africans na timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Kelvin
Yondani anaendelea vizuri japo atakaa nje kwa muda wa wiki mbili mara baada ya
kuanza kupata matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kitengo cha mifupa
(MOI) jijini Dar es Salaam.
Akiongea na mtandao wa klabu
www.youngafricans.co.tz, Daktari wa timu ya Young Africans Dokta Suphian Juma,
amesema Yondani alipata mshtuko katika mfupa wake mkubwa, baada ya kuchezewa
vibaya na kiungo wa timu ya Simba Haruna Moshi 'Boban'.
Dk. Suphian anawatoa wasiwasi
wapenzi na washabiki wa Young Africans, kwamba Yondani anaendelea vizuri na
anatazamiwa kurudi dimbani baada ya wiki mbili. "Unajua Yondani baada ya
kukanygwa na Boban alipata mshituko katika mfupa wake mkubwa mguuni, hivyo
anapata matibabu ya kumrejesha katika hali yake ya kawaida." Alisema Dk.
Suphian.
Katika hali ya kushangaza mwamuzi wa
mchezo huo wa watani wa jadi, Mathew Akrama alishindwa kumonyesha kadi nyekundu
Boban kwa mchezo mbaya uliopelekea Yondani kutolewa nje na kushidwa kuendelea
na mchezo.
Mechi hiyo ya Ligi Kuu ya Vodacom
iliyowakutanisha watani wa jadi wakongwe Afrika Mashariki iliishia kwa sare ya
mabao 1-1, mabao yaliyofungwa na Amri Kiemba Simba dakika ya 4 na Said
Bahanunzi aliyesawazisha kwa upande wa Young Africans dakika ya 67.
Young Africans leo imeendelea na
mazoezi katika uwanja wa shule ya sekeondari ya Loyola kujiandaa na mchezo
unaofuata dhidi ya timu ya Kagera Sugar, mchezo utakaofanyika siku ya Jumapili
katika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba. SOURCE: GLOBAL PUBLISHERS
No comments:
Post a Comment