Monday, October 22, 2012

WAENDA UINGEREZA KUONA BARCLAYS PREMIER LEAGUE

Tunu Kavishe, (Katikati), Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano benki ya Barclays-Tanzania, akizungumza muda mfupi kabla ya kuchezeshwa bahati nasibu ya promosheni ya Barclays ya shinda na ukaone ligi kuu ya Uingereza,  Katika bahati nasibu hiyo, mteja wa benki hiyo jijini Mbeya, Anthony Hancy, aliibuka mshindina hivyo kujipatia nafasi ya kusafiri kwenda uingereza akiwa na ampendaye ili kujionea ligi kuu ya nchi hiyo maarufu kama, "Barclays Premier League". 

Afisa Mawasiliano wa benki ya Barclays, Lillian akichagua kikaratasi wakati wa kuchezeshwa kwa bahati nasibu hiyo iliyosimamiwa na mkaguzi kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha, Bakar Majjid, (Kulia). Bahatinasibu hiyo ilichezeshwa Jumatatu Oktoba 22, 2012 kwenye tawi la benki hiyo, Kijitonyama jijini Dar es salaam

No comments:

Waziri Kombo akutana na Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Umoja wa Afrika

   Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo amekutana na Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa U...