Friday, September 28, 2012

TASWIRA ZA JINSI WAMACHINGA WALIVYOVAMIA NA KUGAWANA NA KUJENGA VIBANDA VYA KUENDESHA BIASHARA ZAO MJINI ARUSHA JANA

Vibanda vya wafanyabiashara wadogo (Wamachinga) walivyojenga baada ya kuvamia na kujipimia maeneo. Hapa vibanda hivyo vinaonekana kuwa tayari kwa biashara zao.
Wanamama wanaouza mboga mboga ambao walikuwa sehemu ya Wamachinga waliovamia uwanja huo, wakiendelea na biashara zao baada ya kujigawia maeneo.
Wamachinga jiji la Arusha waliokosa eneo kwenye uwanja wa NMC jana wakigawana maeneo baada ya kuvunja uzio wa bati uliokuwa umezungushiwa kwenye uwanja ambao awali ulikuwa unamikiwa na Manispaa ya Arusha kabla ya kuuzwa kwa mtu binafsi karibu na Soko la Kilombero, Kata ya Ngarenaro.
 Wamachinga jiji la Arusha waliokosa eneo kwenye uwanja wa NMC jana wakigawana maeneo baada ya kuvunja uzio wa bati uliokuwa umezungushiwa kwenye uwanja ambao awali ulikuwa unamikiwa na Manispaa ya Arusha kabla ya kuuzwa kwa mtu binafsi karibu na Soko la Kilombero, Kata ya Ngarenaro.
 Wamachinga jiji la Arusha waliokosa eneo kwenye uwanja wa NMC jana wakigawana maeneo baada ya kuvunja uzio wa bati uliokuwa umezungushiwa kwenye uwanja ambao awali ulikuwa unamikiwa na Manispaa ya Arusha kabla ya kuuzwa kwa mtu binafsi karibu na Soko la Kilombero, Kata ya Ngarenaro.
 Polisi wakiwa kwenye magari yao baada ya kufika, kuegesha magari yao upande wa pili wa barabara kwenye kituo cha mafuta kwa muda, kisha kuondoka bila kutawanya wafanyabiashara wago (Wamachinga) waliovamia na kujitwalia eneo hilo.
Polisi wakiwa kwenye magari yao wakifika na kuyaegesha magari yao upande wa pili wa barabara kwenye kituo cha mafuta kwa muda kabla ya kuondoka bila kufanya juhudi zozote za kuwazuia machinga hao kujitwalia eneo hilo.Picha na Grace Macha-
----
Na Mahmoud Ahmad-Arusha

 Hali si shwari katika jiji la Arusha na viunga vyake baada ya wafanyabiashara ndogo ndogo maarufu kama wamachinga kuzua tafrani mara walipovamia eneo la kiwanja cha Ermoil lililopo mkabala na soko la Kilombero na kisha kuanza kugawana maeneo ya kufanyia biashara kwa kujipimia.

Vurugu hizo zimetokea jana wakati Rais Jakaya kikwete akiwa jijini Arusha kufungua mkutano mkubwa wa mapinduzi ya kijani ambao umehudhuriwa na wageni mbalimbali kutoka nchi za Afrika,Amerika,Ulaya na Asia. Hatahivyo,katika vurugu hizo mfuasi mmoja wa chama cha     wananchi(Cuf),Athuman Abrahaman alishambuliwa kwa mawe na kisha kujeruhiwa eneo la usoni na watu wanaodhaniwa kuwa ni wafuasi wa Chadema huku gari la matangazo la Cuf nalo likijikuta likipopolewa kwa mawe na spika zake kuharibika vibaya. Askari wa jiji la Arusha walionekana majira ya saa 3;30 asubuhi akipita na gari lao katika maeneo mbalimbali ya jiji hapa huku wakiwatangazia wamachinga wote kuondoka katika maeneo ambayo hayajatengwa kufanyia biashara zao. 

Askari hao walikuwa wakiwatangazia wamachinga hao kuondoka katika maeneo ambayo hayajatengwa kufanyia biashara huku wakitamka ya kwamba endapo wakikahidi watachukua bidhaa zao kwa nguvu na kuwachukulia hatua za kisheria. Hatahivyo,baada ya muda mfupi ndipo askari hao wali anza kutekeleza majukumu yao ya kusomba bidhaa hizo na kisha kuzipakia ndani ya gari lao huku wakivipeleka katika ofisi za manispaa ya Arusha. 

Hatua hiyo iliwapelekea wamachinga hao kujikusanya kwa pamoja na kisha kuvamia ghafla eneo la wazi wa Ermoil kwa kuvunja uzio wa mabati uliokuwepo na kisha kuanza kujigawia maeneo kwa kuyapima kwa kamba. Wamachinga hao zaidi ya 200 walivamia huku wengine wakitumia nafasi hiyo kupora mali mbalimbali zilizopo ndani ya eneo hilo kama mabati,nondo na saruji zilizokuwa ni mali za mtu anayedaiwa kumiliki eneo hilo. Katika heka heka za kugawana viwanja ndani ya eneo hilo wamchinga hao walikata miti iliyokuwemo ndani na kisha kuanza kuichoma kwa moto hali ambayo ilisababisha wingu zito la moshi kutanda hewani.

 Hatahivyo,wakati tafrani hiyo ikiendelea polisi waliokuwa wamesheheni kwenye magari yao walikuwa wakipita mara kwa mara kuzunguka eneo hilo lakini hawakuonekana wakifanya udhibiti wowote zaidi ya kuwaangalia wamachinga hao. Kitendo cha askari wa jeshi la polisi mkoni hapa kushindwa kuwadhibiti wamachinga hao kimetajwa kimetokana na uhaba wa askari kutokana na ugeni wa mkutano wa jana pamoja na kuhofia hali ya amani kuharibika jijini Arusha.

Mkuu wa wilaya ya Arusha,John Mongella alilaani tukio hilo na kusema kwamba wamachinga hao wamevamia eneo hilo kimakosa kwa kuwa si la kwao huku akikitupia lawama chama kimoja cha siasa hapa nchini kwamba kimehusika katika kuhamasisha vurugu hizo. Alisema kwamba kwa sasa watakutana kujadili tukio hilo kwa undani kwa kuwa wana ugeni mkubwa lakini alisema kwamba kitendo cha wafuasi wa Chadema kupiga mawe gari la Cuf na mfuasi wake si cha kiungwana. 

Kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa ya jiji la Arusha,Omary Mkombole alisema kwamba kitendo cha wamachinga hao kuvamia eneo hilo ni kuvunja sheria na wataondolewa hapo hivi karibuni. Mkombole,mbali na kulaani tukio hilo alisema kwamba uongozi wa jiji umepanga maeneo mbalimbali ya kufanyia biashara na eneo hilo ni mali ya mtu binafsi ambapo alikuwa ameanza jitihada za kuliendeleza.

No comments: