Tuesday, September 15, 2009

Ufisadi mpya BoT


VIGOGO wanne wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam wakikabiliwa na shtaka la Uhujumu Uchumi na kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya Sh104 bilioni.

Vigogo hao ambao wote ni wakurugenzi wa BoT wa vitengo tofauti, walifikishwa mahakamani hapo asubuhi chini ya ulinzi mkali wa polisi.

Wameshtakiwa chini ya Sheria ya Uhujumu Uchumi ya mwaka 2002.

Wakurugenzi hao wanashtakiwa kwa makosa tofauti ikiwamo kosa la tatu linalowahusisha wote wanne ambao ni Mkurugenzi wa Benki ya BoT, Simon Eliezer Jengo, Naibu Mkurugenzi wa Fedha wa benki hiyo Kisima Thobias Mkango, Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Sheria Bosco Ndimbo Kimela na Mkurugenzi wa benki, Ally Farijallah Bakari.

Mwendesha mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Benny Lincon alimwambia hakimu Samuel Maweda kuwa vigogo hao wanne, wakiwa watumishi wa umma walitenda makosa hayo kwa nyakati tofauti na kuisababishia serikali hasara ya Sh104,158,536,146.

“Kwa pamoja na kwa makusudi walishindwa kuchukua tahadhari au kusahau majukumu yao katika mazingira nyeti, kwa udanganyifu walitayarisha nyongeza kwenye mkataba wa 2001 unaohusiana na uchapaji wa noti za benki kwa gharama kubwa ambapo bei ya mkataba huo iliisababishia serikali hasara ya Sh104,158,536,146,” alidai Licon.

Licon aliendelea kuieleza mahakama kuwa mwaka 2004 washtakiwa Jengo na Mkango wakiwa ndani ya jiji na Mkoa wa Dar es Salaam na wakiwa wameajiriwa katika utumishi wa umma katika nyadhifa tofauti ndani ya BoT, kwa pamoja na kwa makusudi, wakiwa na lengo la kuvunja kanuni walitangulia kutoa ofa kwa wasambazaji wa noti za benki.Pauline Richard na Salim Said.

No comments: