MOHAMED Mpakanjia, ambaye alikuwa mume wa mbunge viti maalum kwa tiketi ya CCM, marehemu Amina Chifupa, amefariki dunia ikiwa ni takriban miaka miwili tangu mkewe aage dunia.
Mpakanjia, ambaye alikuwa mfanyabiashara maarufu jijini Dar es salaam, alifariki dunia jana alasiri akiwa hospitali ya Lugalo jijini Dar es salaam inayomilikiwa na Jeshi la Wananchi (JWTZ).
Kifo cha Mpakanjia kimetokea takribani miaka miwili na miezi kadhaa tangu mkewe Amina Chifupa, ambaye aliibukia kwa nguvu kwenye siasa na kuzimika ghafla, kufariki dunia katika hospitali hiyo Juni 27, 2007 baada ya kusumbuliwa na homa ya kisukari na malaria.
Habari kutoka kwa watu wa karibu na marehemu zinasema kuwa Mpakanjia, ambaye alikuwa akimiliki alifikishwa katika hospitali ya Lugalo juzi usiku baada ya kusumbuliwa na homa ya Pneumonia.
Comments
UKIMWI UTATUMALIZA - TUWENI MAKINI...KUWA NA MMOJA MWAMINIFU, KONDOMU...KUTAHIRI - TUJARIBU KILA SILAHA....CHANJO NDIYO HIYO WATAALAMU
WANASEMA KWAMBA ITACHUKUA MIAKA MITANO IJAYO. LET US HANG IN THERE. TUWE WAANGALIFU JAMANI