Tuesday, September 08, 2009

Makumbusho ya zama za mawe za kale za Isimila hatarini kutoweka









ZAMA za mawe za kale na nguzo za asili za Isimila zilizo katika kijiji cha Ugwachanya, ni miongoni mwa Vivutio vinavyoupamba Mkoa wa Iringa.
Zama hizo zinakadiliwa kuishi miaka laki tatu hadi laki nne kabla ya kristo, na ziligunduliwa na wenyeji wa eneo hilo kabla ya kufanyika utafiti mwaka 1951 kisha eneo hilo kutangazwa rasmi kwamba lina utajiri wa masalia ya zama hizo .
Miongoni mwa zama zilizo katika Korongo la Isimila lenye mikondo miwili, ni Mikuki iliyotumika kwa ajili ya kujihami na mawe ya kombea kwa ajili ya kazi ya uwindaji.
Nyundo zilizokuwa zikitumika kwa ajili ya kutengenezea zama nyingine na Shoka mahususi kwa kazi ya kuvunja mifupa, Vyembe na visu. Taarifa ya Tumaini Msowoya.

No comments:

SADC Yazindua Mkakati wa Mawasiliano wa mwaka 2025-2030

Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) imezindua Mkakati wa Mawasiliano na Uhamasishaji wa Mwaka 2025-2030 ili kuimarisha mawasiliano...