NEW YORK, Marekani
Kiongozi wa Libya Kanali Muammar Gaddafi amehutubia mkutano wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa wa kila mwaka akasema kuwa Umoja huo wa mataifa hauko fair kwanza unajali nchi tajiri kuliko masikini, unasimamia mambo ya ajabu, vita 65 vimeshatokea bila ya idhini ya UN. Kama mzaha vile akatishia kutaka kuchana charter ya UN.
Anasema Marekani wala siyo sehemu nzuri, ni kama vile jela ya Guantanamo, sababu kuna mikwala mingi ili kuingia
kwanza daktari wake kanyimwa viza, halafu alikwenda na ndege zake tatu lakini wakamlazimisha aongezewe rubani mmoja wa akiba wa ndege yake wakati yeye anao marubani wataalamu.
Kisha ametaka mataifa tajiri yaziheshimu nchi masikini na pia hatua kali zichukuliwe kwa mataifa yanayokiuka
alipofika Marekani amekataa kupangiwa katika hoteli yoyote ile badala yake ametafuta sehemu akasimika mahema yake, marekani imemkatalia.
Sasa anataka Afrika ipewe kiti cha kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Anapinga kabisa mfumo uliopo wa Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa.
Tayari Rais Barack Obama wa Marekani ameshahutubia UN na ameitaka Jumuiya ya Kimataifa kujihusisha kwa vitendo, akisema Marekani pekee yake haiwezi kutatua migogoro na changamoto zote zinazoukabili ulimwengu.
Akizungumza katika hotuba yake ya kwanza katika kikao cha mkutano wa baraza kuu la umoja wa Mataifa mjini New York, Obama alisema wenye uzoefu wa kuitia adabu Marekani kwa madai ilibeba mzigo wa ulimwenguni pekee yake, wakati huu hawawezi kukaa kando wakisubiri Marekani itatue matatizo yote ya ulimwengu.
Obama alitoa mfano wa hali mbaya ulimwengu utajikuta iwapo jumuiya ya kimataifa haitoshirikiana kutatua matatizo mengi. Rais huyo wa Marekani alisema kuna uwezekano wa makundi yenye siasa kali kuongezeka, vita na mizozo kuzidi, pamoja na mauaji ya halaiki.
Swala la nchi nyingi kujipatia silaha za nuklia, ongezeko la ujoto duniani kufuatia mabadiliko ya hali ya hewa, umaskini na kuongezeka kwa maradhi pia ni mifano Obama ilitoa endapo jumuiya ya kimataifa haitashikana mikono kushirikiana. Kiongozi wa Libya Kanali Muammar Ghadaffi pia alikihutubia kikao hicho cha baraza kuu la Umoja wa Mataifa kwa mara ya kwanza.
Comments