KESI ya matumizi mabaya ya ofisi yaliyoisababishia serikali hasara ya zaidi ya Sh 11 bilioni inayowakabili mawaziri wa zamani Basil Mramba, Daniel Yona na Katibu Mkuu Mstaafu wa wizara ya Fedha na Uchumi Gray Mgonja inatarajiwa kuendelea kusikilizwa kwa awali Septemba 16 mwaka huu.
Hayo yalielezwa jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na Hakimu Mkazi Eva Nkya wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa.
Mara ya mwisho kesi hiyo ililazimika kuahirishwa baada ya kuharibika kwa kompyuta iliyokuwa ikirekodi mwenendo mzima wa kesi hiyo.
Washitakiwa hao wanadaiwa kuwa wakiwa waajiriwa wa serikali walitumia madaraka yao vibaya kwa kuipatia msamaha wa kodi kampuni ya M/S Alex Stewart na kuisababishia hasara serikali ya kiasi hicho cha pesa.
Comments