Taarifa ambazo ambazo haziridhishi kabisa kuamini zimetufikia jana usiku kutokea Dodoma ambapo pia iliitishwa Press Conference usiku huo huo Slaa mwenyewe akidai kuwa aliwekewa vifaa vivyo vya kurekodi sauti. Mambo mawili ambayo naungana na ndugu yangu Maro inasikitisha kwamba tumeingia kwa mkumbo kwa mawazo ya kulia tu ni haya.
1.Kwanini tunashikilia Dk Slaa ndiyo amewekewa vifaa hivyo na watu ambao hawatuwafahamu ili khali inawezekana kabisa Dk Slaaa na CHADEMA wakawa wameweka vifaa hivi kama kujitafutia Umaarufu. Hilo Linawezekana na ni moja ya mbinu za kisiasa ili watu waendelee kuamini kuwa unaweza kuleta Mabadiliko. Tusubiri uchunguzi na iiwezekana Mzee Mwanakijiji na Bongo Radio any mahojiano na wale wahudumu wa ile Hotel.
2.Kuanza kuhisi kuwa ni Masha ndiyo kafanya jmbo hili,ama waziri kijana.Huu ni upotoishaji tena kwa hoja kwamba Masha alilipuliwa na Dr. Slaa. Kama tumefika katika siasa za chuki kama alivyosema Mzee Mkapa basi 2010 uchaguzi utakuwa ni wa aina ya ajbu kutokea katika Nchi hii.
2009/2/6 Josephat Isango
Watanzania ambao kwa muda huu mmelala fofofo, muda huu ni Saa saba Usiku, Dodoma hali sio nzuri usiku wa leo, Dr, wilbrod Slaa na Tarab Ally wamewekewa vitu vinavyosadikiwa kuwa ni vifaa vya kuwarekodi kwenye vyumba vyao vya kulala, kwenye sehemu za uvungu wa vitanda. hatujajua lengo la watu hao kuweka vifaa hivyo, ila ninachoweza kusema ni wabunge ambao wamekuwa na changamoto Bungeni, huenda kuna njama za Wabunge hao kuhujumiwa. Nchi yetu sijui inaenda wapi tuiombee.
Comments
Dr. Slaa aluta continua!!