Wednesday, February 04, 2009

Nora bwana na mambo yake




KAMPUNI ya Beknet Tanzania Limited imeandaa uzinduzi wa albamu ya Upande wa Pili wa Ndoa isiyo ya Uaminifu katika Ukumbi wa Cinema wa Century Cinemax Mlimani City Februari 6.

Akizungumza na Mwananchi jijini jana, mkurugenzi wa filamu hiyo, Bariki Keenja alisema anatarajia uzinduzi wake utafana kwani katika filamu yake kuna mengi ya kufurahisha.

Alisema katika filamu hiyo, imezungumzia maisha halisi ambayo yapo katika jamii ya sasa ambapo mwanamke au mwanaume kumsaliti mwenzi wake kwa namna moja au nyingine na hii hutokana na tamaa zisizo na msingi.

Filamu hiyo imewashirikisha wasanii mbalimbali akiwemo Nuru Nasoro ''Nora'', Elizabeth Chijumba ''Nikita'', Ahmed Olotu anayetambulika kwa jina la kisanii, Mzee Chilo na Subira Maulid.

Pichani kulia Nora akisikiliza swali kwa makini kutoka kwa mmoja wa waandishi wa habari alipomuuliza kuhusiana na habari za kashfa ambazo zimekuwa zikimuandama muigizaji huyo juu ya mapenzi na wanaume tofauti tofauti

No comments:

MIAKA 99 YA JESHI LA CHINA IWE CHACHU CHA KUIMARISHA USHIRIKIANO WA ULINZI NA TANZANIA- DKT RHIMO NYANSAHO

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Rhimo Nyansaho (Mb), amesisitiza umuhimu wa kuendeleza ushirikiano kati ya Tanzania na Chin...