Tuesday, February 10, 2009

Jamani waliosoma Milambo huu wimbo mwaukumbuka

Hapa utamkuta Headmaster wetu wakati huo Bw. Anthony Msemakweli enzi hizo tukimwita jina la Fupa, kulia kwake yupo Second Master Mwalimu Kyala ilikuwa matata, lazima kwanza uwe suruali umepiga pasi, nguo safi na hawakuruhusu watu kujongo na huu wimbo uliimbwa mara baada ya watu kupata sifongo au uji wakati huo.

Milambo shule yangu naipenda,

Chorus:Milambo shule yangu naipenda,

Ina michepuo

Chorus: Yenye sifa tele,

Hasa wa lugha,

Chorus: Kingereza, Kiswahili, Kifaransa,

Biashara

Chorus:Na Masomo ya jamii na michezo,

Na Kilimo

Mashambani bustani, ufugaji

Motto wetu siku zote

Chorus: Elimu ni amana, pia ni ufunguo,
huleta ufanisi,
Elimika,

Chorus: aaaa Jenga taifa,

4 comments:

Anonymous said...

Yahya acha hizo, na nyie boys mlikuwa mnaitikia vipi wakati sisi wanaume tukiimba? Au mlikuwa mnawaiga girls?..........

Anonymous said...

Yahaya umenikumbusha mbali sana....Hivi Headmaster wetu Mr. Msemakweli yuko wapi siku hizi?

Those good old days !

Anonymous said...

Halafu kumbe Msemakweli alikuwa mwanamichezo mzuri sana alipokuwa chuo. Angalia link hiyo hapo chini!

http://www.gobadgers.ca/sports/msoc/MVP

Anonymous said...

Naitwa Masabo,
Yahya, nimechelewa sana kusoma hiyo article, lakini umenikumbusha mbali sana... Nilikaa na Msemakweli miaka sita... Nilijifunza mengi na yamenisaidia sana katika masisha yangu, kweli moto wetu siku zote elimika jenga taifa...Lakini sikumbuki kusikia au kuona jina lako pale Milambi, ulikuwa wapi wakati huo?