Taarifa zilizotufikia punde tu zinaeleza kuwa yule gwiji wa muziki wa dansi na ambaye ni mmoja wa visiki vya bendi ya Msondo Ngoma Jazz Band bwana Joseph Maina amefariki dunia akiwa safarini ndani ya daladala akitokea maeneo ya Mbagala. Kwa sasa maiti ya mwanamuziki huyo tunaelezwa iko ndani ya hospitali ya Temeke imeshushwa na wasamaria wema. Maina kwa wale wasiomjua ni mwanamuziki mkongwe na mtunzi wa nyimbo nyingi lakini kubwa ni ile ya Baba Gift habari zaidi tutakuwa tukiendelea kuwaletea.
Comments
Kigali, Rwanda