Zombe amwaga chozi mahakamani

Ajitetea saa tatu

MSHTAKIWA wa kwanza katika kesi ya mauaji ya wafanyabiashara watatu wa madini kutoka mjini Mahenge, Morogoro na dereva teksi wa Manzese jijini Dar es Salaam inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Dar es Salaam Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Abdallah Zombe jana alijikuta akimwaga machozi kizimbani wakati akiwasilisha utetezi wake.

Zombe alijikuta akimwaga machozi mara kadhaa wakati akijitetea mbele ya Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Salum Masatti kuhusiana na tuhuma hizo zinazomkabili yeye pamoja na askari wenzake tisa.

Hatua ya Zombe kupanda kizimbani jana na kuanza kujitetea ilikuja baada ya mahakama hiyo kuridhika kuwa yeye na wenzake wana kesi ya kujibu dhidi ya mauaji ya wafanyabiashara hao kulingana na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo hoja za mawakili wa watuhumiwa hao na majibu ya hoja hizo kutoka kwa upande wa mashitaka. Kwa taarifa zaidi bonyeza hapa

Comments