Friday, February 13, 2009

Mauaji: Baada ya Zombe, Bageni amwaga mboga, ajitetea kwa saa sita



MSHITAKIWA wa pili katika kesi ya mauaji ya wafanyabiashara watatu wa madini na dereva teksi wa Manzese Dar es Salaam, Mrakibu wa Polisi (SP), Christopher Bageni amezidi kumuweka pabaya mshitakiwa wa kwanza katika kesi hiyo, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Abdallah Zombe.


Bageni na wenzake tisa, akiwemo Zombe, wanashitakiwa kwa tuhuma za kuwaua wafanyabiashara watatu wa madini ya rubi kutoka Mahenge mkoani Morogoro- Sabinus Chigumbi, maarufu kama Jongo, Ephrahim Chigumbi, Mathias Lunkombe na dereva wa teksi wa Manzese jijini Dar es salaam, Juma Ndugu.


Bageni alidaiwa na Zombe kuwa ndiye aliyeamuru wafanyabiashara hao kuuawa, lakini jana alimshambulia Zombe kuwa muhusika mkuu. Hadi sasa, mtuhumiwa mmoja katika kesi hiyo, Koplo Saad Alawi, ambaye anadaiwa kufyatua risasi na kuwaua wafanyabiashara hao, hajakamatwa.


Katika utetezi huo uliodumu kwa saa sita, Bageni aliieleza Mahakama Kuu kuwa Zombe alimrubuni kuwa wapeleke taarifa ya uwongo kwenye tume ya Jaji Musa Kipenka, iliyoundwa na Rais Jakaya Kikwete kuchunguza ukweli wa vifo vya wafanyabiashara hao.


Mbele ya Jaji Salum Massatti anayeisikiliza kesi hiyo, Bageni alidai kuwa Zombe alimweleza kuwa walisoma na Jaji Kipenka darasa moja katika Shule ya Sekondari Songea na kwamba ameahidi kuwasaidia katika suala la mauaji hayo.


“Mshitakiwa wa kwanza aliniambia kuwa Jaji Kipenka ni “classmate” wake... walisoma naye darasa moja Songea Boys na kwamba wamewasiliana na amemwambia kuwa tupeleke taarifa iliyorekebishwa ili awasaidie vijana wetu,” alidai Bageni wakati akijibu maswali kutoka kwa wakili wa serikali, Angaza Mwipopo.


Bageni alidai kutokana na ushauri huo wa Zombe waliamua kuibadili taarifa waliyoipeleka kwenye tume hiyo, tofauti na taarifa waliyoiandaa ambayo ilipelekwa katika kitengo cha uhalifu, maarufu kama 99. Taarifa nyingine cheki hapazaidi

No comments: