Tuesday, February 24, 2009

Liyumba apatikana azuka mahakamani

Picha ya Bongo pix
Mkurugenzi wa zamani wa utawala na utumishi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Amatus Liyumba, ambaye anadaiwa kutoweka, litajulikana leo wakati kesi inayomkabili ya tuhuma za kutumia vibaya madaraka na kuisababishia serikali hasara ya Sh 221 bilioni, ameonekana leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Kisutu.

Liyumba ameingia mahakamani hapo akiwa katika gari lake binafsi la kifahari na alishuka katika gari lake bila ya wasi tofauti na ilivyokuwa ikiriupotiwa ya kwamba mtuhumiwa huyo alikuwa akitafutwa kwa udi na uvumba. Kupatikana kwake kumeondoa utata uliokuwapo siku za nyuma kuhusu kuwapo au kutoroka kwake.

Alikuwa akisakwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), muda mfupi baada ya kupewa dhamana katika mazingira yenye utata na taasisi hiyo, ambayo sasa ina uwezo wa kuendesha kesi, ilipewa kibali cha kumkamata, lakini ilishindwa kumtia nguvuni na hivyo kusababisha uvumi kuwa mtuhumiwa huyo ametoweka.

Mtuhumiwa huyo, ambaye ameshtakiwa kwa pamoja na Deogratius Kweka ambaye bado yuko ndani, alimudu kutoka mahabusu baada ya mahakama kukubali hati moja yenye mali za thamani ya Sh882 milioni katika dhamana ya thamani ya Sh55 bilioni, baada ya hati kadhaa kuonekana kuwa na kasoro, ikiwemo ya kusafiria ambayo ilionekana kuisha muda wake. Taarifa zaidi bidae.

No comments: