Thursday, February 19, 2009

Liyumba aponyoka



KAMANDA Amatus Liyumba aliyekuwa Mkurugenzi wa utawala wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), ametoweka na hajulikani alipo mpaka sasa kiasi kwamba Taasisi ya Kuzuia na kupambana na rushwa (PCCB) imeiomba mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu itoe hati ya kukamatwa kwake siku mbili baada ya kumwachia kwa dhamana.

Hati ya kukamatwa Liyumba na wadhamini wake wawili, ilitolewa juzi na hakimu Mkazi anayesikiliza kesi hiyo, Khadija Msongo.

Wakati Liyumba bado hajakamatwa, wadhamini wake jana walikamatwa na kuwekwa mahabusu ingawa baadaye waliachiwa baada ya hakimu kudai kuwa hawezi kutoa uamuzi wowote kutokana na jalada la kesi hiyo kuitishwa mahakama kuu.
Hakimu Msongo aliwataka wadhamini hao kufika mahakamani leo ambapo atatoa uamuzi.

Mwendesha Mashataka wa TAKUKURU, Tabu Mzee aliieleza mahakama kuwa juzi na jana, Liyumba ambaye ni mshtakiwa namba moja katika kesi ya kuisababishia serikali hasara ya Sh221 bilioni, hakuweza kupatikana kwa simu wala nyumbani kwake.

Liyumba na mwenzake Deogratias Kweka, walifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Januari 27 mwaka huu na kurudishwa rumande baada ya kushindwa kutoa Sh55 bilioni taslimu au hati ya mali isiyohamishika yenye thamani hiyo. Taarifa kwa kina soma www.mwananchi.co.tz

No comments: