WAZIRI WA MICHEZO ARIDHISHWA NA UKARABATI UWANJA WA NYAMAGANA JIJINI MWANZA. KAMPUNI YA MAFUTA MOIL YAONESHA NIA YA KUWEKA MAJUKWAA
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (wa nne kulia), akiteta jambo la Afisa Habari, ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Atley Kuni (wa tatu kushoto) alipotembelea uwanja mkongwe wa Nyamagana Jijini Mwanza hii leo ili kujionea zoezi la uwekaji wa nyasi bandia kwenye uwanja huo.
Waziri Nhauye ameeleza kuridhishwa na uwekaji wa nyasi bandia kwenye uwanja huo ambapo amewashukuru wadau wote waliofanikisha ukarabati wake wakiwemo wajasiriamali Jijini Mwanza ambao kodi zao zimesaidia upatikanaji wa zaidi ya shilingi Milioni 190 kutoka Halmashauri ya Jiji hilo ambazo zilizojumuishwa na dola za Kimarekani Laki Tano zilizotolewa na Shirikisho la Soka Duniani FIFA kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo.
Altaf Hiran Mansoor ambaye ni mdau wa michezo Jijini Mwanza na Mkurugenzi wa Kampuni ya Mafuta ya MOIL, amesema kampuni hiyo iko tayari kuchangia ukarabati wa uwanja huo ikiwemo ujenzi wa majukwaa.
Na BMG
Itakumbukwa kwamba nyasi bandia kwa ajili ya uwanja huu zilikwama bandarini kwa muda mrefu baada ya TFF kutakiwa kulipiwa kodi ya zaidi ya shilingi Milioni 32 hali ambayo ilisababisha utekelezaji wake kusuasua.
Waziri Nape Nhauye amesema Serikali itaendelea kuboresha viwanja mbalimbali nchini ikiwemo kushirikiana na makampuni mbalimbali ili kukarabati viwanja vilivyopo ili Tanzania iwe sehemu bora hata kwa mataifa mengine kufika kwa ajili ya mazoezi na michezo mbalimbali hususani ya mpira wa miguu.
Altaf Hiran Mansoor ambaye ni mdau wa michezo Jijini Mwanza na Mkurugenzi wa Kampuni ya Mafuta ya MOIL, amesema kampuni hiyo iko tayari kuchangia ukarabati wa uwanja huo ikiwemo ujenzi wa majukwaa.
Wadau wa michezo Jijini Mwanza wamefurahishwa na uwekaji nyasi kwenye uwanja mkongwe wa Nyamagana ambao ulianzishwa mwaka 1945 ambapo wamesema utaongeza chachu ya ongezeko la mechi za mpira wa miguu Jijini Mwanza pamoja na kuongeza vyanzo vya mapato pia.
Uwanja mkongwe wa Nyamagana sasa unang'aa kwa viwango vingine, ambapo Waziri Nape amesema anashawishika kuandaa mechi ya kirafiki kati ya timu za Simba na Yanga zinazoundwa na wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, itakayochezewa kwenye uwanja huo.
Itakumbukwa kwamba Mwaka 1974 timu za Simba na Yanga zilikutana kwenye uwanja wa Nyamagana, kwenye Fainali ya Ligi ya Taifa ya Soka ambapo Yanga iliichapa Simba bao 2-1
Mwonekano wa Uwanja wa Nyamagana Jijini Mwanza baada ya kuwekewa nyasi bandia
Comments