Tuesday, November 22, 2016

TEA NA CRDB YAKABIDHI VITANDA NA MAGODORO SHULE YA SEKONDARI PANGANI

 Meneja Elimu, Habari na Mawasiliano wa Mamlaka ya Elimu Tanzania Bi. Sylvia Lupembe akisaini kitabu cha wageni wakati wa hafla ya kukabidhi Vitanda vya double deka 24 na Magodoro 48  kwa ajili ya bweni la wanawake kwenye shule ya sekondari Pangani iliyopo Wilayani Kibaha mkoani Pwani.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha Bi. Rosemary Msasi akongea wakati wa hafla ya kukabidhi Vitanda vya double deka 24 na Magodoro 48  kwa ajili ya bweni la wanawake kwenye shule ya sekondari Pangani  ambapo alisema kuwa ujenzi wa miundombinu hiyo kwa kiasi kikubwa utasaidia kuinua kiwango cha elimu kwa mtoto kike na kuwawezesha kufanya vizuri katika mitihani yao.
Meneja Elimu, Habari na Mawasiliano wa Mamlaka ya Elimu Tanzania Bi. Sylvia Lupembe akiongea wakati wa hafla ya kukabidhi Vitanda vya double deka 24 na Magodoro 48  kwa ajili ya bweni la wanawake kwenye shule ya sekondari Pangani na kuwataka wanafunzi watakaotumia bweni hilo kuvitunza vifaa hivyo ili viweze kudumu ili kuwawezesha wengine kulitumia.
 Meneja wa CRDB tawi la Kibaha Bi. Rosemary Nchimbi akisoma taafifa fupi wakati wa hafla ya kukabidhi Vitanda vya double deka 24 na Magodoro 48  kwa ajili ya bweni la wanawake kwenye shule ya sekondari Pangani ambapo alisema kuwa lengo la kutoa msaada wa vifaa hivyo ni kwa ajili ya kusaidia kutatua changamoto zilizokuwa zikiwakabili watoto wakike katika shule hiyo ikiwamo kusafiri umbali mrefu kuja shuleni.
Kaimu Katibu Tawala Wilaya ya Kibaha Bw. Anathory Mhango akiongea wakati wa hafla ya kukabidhi Vitanda vya double deka 24 na Magodoro 48  kwa ajili ya bweni la wanawake kwenye shule ya sekondari Pangani ambapo alisema kuwa  anaamini lengo la mradi huo lenye dhumuni ya kumuendeleza mtoto wa kike litasaidia kuondo chagamoto zilizokuwa zikiwakabili watoto wa kike kwa muda mrefu.


Kaimu Katibu Tawala Wilaya ya Kibaha Bw. Anathory Mhango akiwaonesha Meneja Elimu, Habari na Mawasiliano wa Mamlaka ya Elimu Tanzania Bi. Sylvia Lupembe(mwenye nguo nyeupe) na Meneja wa CRDB tawi la Kibaha Bi. Rosemary Nchimbi (katikati mwenye nguo nyeusi) moja ya bweni la wanawake lenye vitanda na magodoro walivyotoa katika shule ya sekondari pangani mkoani Pwani.
Kaimu Katibu Tawala Wilaya ya Kibaha Bw. Anathory Mhango akiwashukuru Meneja Elimu, Habari na Mawasiliano wa Mamlaka ya Elimu Tanzania Bi. Sylvia Lupembe (mwenye nguo nyeupe) na Meneja wa CRDB tawi la Kibaha Bi. Rosemary Nchimbi (katikati mwenye nguo nyeusi) kwa masaada wa vitanda 24 na magodoro 48 yaliyogharimu milioni 18 kwa ajili ya bweni la wanawake kwenye shule ya sekondari Pangani iliyopo Wilayani Kibaha mkoani Pwani.
Meneja Elimu, Habari na Mawasiliano wa Mamlaka ya Elimu Tanzania Bi. Sylvia Lupembe na Meneja wa CRDB tawi la Kibaha Bi. Rosemary Nchimbi  wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi,walimu na viongozi wa mkoa wa Pwani wakati wa hafla ya kukabidhi Vitanda vya double deka 24 na Magodoro 48  kwa ajili ya bweni la wanawake kwenye shule ya sekondari Pangani iliyopo Wilayani Kibaha mkoani Pwani.

(PICHA NA KITENGO CHA HABARI, ELIMU NA MAWASILIANO MAMLAKA YA ELIMU TANZANIA)

No comments: