Monday, November 07, 2016

SAMWEL SITTA, "MZEE WA SPEED NA VIWANGO" HATUNAYE TENA DUNIANI, AFARIKI DUNIA AKIWA KWENYE MATIBABU UJERUMANI

 Spika wa bunge mstaafu, Samwel Sitta, au kama alivyojiita "Mzee wa Speed na Viwango" amefariki dunia usiku wa kuamkia leo akiwa nchini Ujerumani alikopelekwa kupatiwa matibabu. Taarifa iliyotolewa na mwanaye Benjamin Sitta, ambaye ni Meya wa Manispaa ya Kinondoni, mapema leo aimethibitisha kifo cha Mzee Sitta. Tayari Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, amemtumia salamu za rambirambi spika wa bunge Job Ndugai, kufuatia kifo cha mzee Sitta. Kwa muda mrefu Mzee Sitta ambaye aliwahi kutumikia nyadhifa mbaklimbali tangu serikali ya awamu ya kwanza, alikuwa haonekani hadharani kutokana na kuugua. Ni miezi michache iliyopita Mzee Sitta alikuwa akionekana kwenye vyombo vya habari akitembeelwa na viongozi mbalimbali kumjulia hali. Munhu aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi AMIN.
 
 Mzee Sitta akiwa na mkewe, Mamam Margaeth Sitta wakati wa uhai wake
 Spika sitta, akipokea ripoti maarufu ya Richmond, kutoka kwa mwenyekiti wa kamati teule, Dkt. Harrison Mwakyembe. Ripoti hii ilimuondoa madarakani aliyekuwa Waziri Mkuu wakati wa kuingia kwa serikali ya awamu ya nne, Edward Lowassa.
 Mzee Sitta alikuwa rafiki wa kila mtu. Hapa akiwa na Mbunge Tundu Lissu kutoka CHADEMA

 Spika Sitta, akila kiapo cha kushika uspika wa bunge, mwanzoni mwa serikali ya awamu ya nne

No comments: