









Na Dustan Shekidele, Morogoro.
HATIMAYE baada ya ukarabati wa takribani miaka miwili, hatimaye Stendi ya Mabasi ya Mikoani ya Msamvu iliyopo Morogoro imefunguliwa mwishoni mwa wiki iliyopita huku ikiwa na muonekano wa kisasa kabisa na wengine kuifananisha na uwanja wa ndege ‘Airport’.
Leo asubuhi tovuti yetu imetinga ndani ya stendi hiyo ya kisasa ambayo iko kwenye hatua za mwisho za kumalizia ukarabati kwa kiwango cha hali ya juu, ambapo picha zilizopigwa zinaonesha namna ambavyo mandhari ya stendi hiyo yanavyovutia kwa sasa tofauti na ilivyokuwa awali kabla ya ukarabati.
Wameshuhudiwa abiria wengi wakipanda na kushuka kwenye mabasi kama wako uwanja wa ndege huku wengine wakisubili usafiri ili kuelekea sehemu mbalimbali.
Akizungumza na mwandishi wetu, mmoja wa viongozi wa Stendi hiyo, ameeleza kuwa, endapo wakimkamata mtu yoyote akitupa takataka ama kukanyaga bustani atatozwa faini ya Tsh. 50,000/= papo hapo.
No comments:
Post a Comment