RC GAMBO AZINDUA DARAJA LA MTO KIJENGE


Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe Mrisho Gambo akizungumza na wananchi wa Kata ya Engutoto na Moshono wakati wa Uzinduzi wa Daraja la Mto Kijenge 
Mkuu wa wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo(kwanza kulia) akizungumza na wadau wa maendeleo Bw. Hans Paul(pili kulia) na Bw. Bw. Jagjit Aggarwal
 Daraja walilokuwa wanatumia wananchi wa Engutoto na Moshono kabla ya kujengewa Daraja la kiwango na Kampuni ya Dharam Sign Hanspaul 
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo akizindua Daraja la Mto Kijenge Hili ndilo Daraja lililojengwa na wafadhili chini ya Bw. Hans Paul lina upana wa Mita 20, uwezo wa kupitisha magari yenye uzito wa Tani 3, urefu kwenda juu Mita 2.2 na uwezo wa kudumu kwa miaka 50.

Katibu Tawala wa Wilaya ya Arusha Ndg. David Mwakiposa akimkaribisha Vongozi wa Serikali na wananchi wa Kata ya Engutoto kwenye uzinduzi wa daraja la Mto Kijenge lililojengwa kwa ufadhili wa Dharam Singh Hanspaul
Kijenge
Wakazi wa Kata za Engutoto na Moshono wakitoa shukrani zao kwa kukabidhi Mbuzi na kumvika mavazi ya kimaasai Mfadhili aliwajengea Daraja la Mto Kijenge Bw. Hans Paul 

Diwani wa Kata ya Engutoto kwa kupita Tiket ya Chadema Mhe.Aman Reward alishirki katika uzinduzi wa Daraja na kupongeza Viongozi wa Mkoa na Jiji kwa namna wanavyowatumika wananchi
Diwani wa Kata ya jirani ya Themi kupitia Tiketi ya Chadema Mhe. Melance Kinabo pia alishirki katika uzinduzi wa Daraja la Mto Kijenge.


Nteghenjwa Hosseah - Arusha


Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo amezinduzaa daraja la Mto Kijenge linalounganisha kata za Engutoto na Moshono ambalo limejengwa kwa ufadhili wa Kampuni ya Dharam Singh Hanspaul.

Akizungumza katika uzinduzi huo Mkuu wa Mkoa amesema daraja hilo ni ukombozi na msaada kwa wananchi wengi ambao walikua wakipata adha kubwa ya kuvuka haswa wakati wa mvua kutokana na kukosa kivuko cha uhakika na kivuko kilichokuwepo awali kiliashiria hali ya hatari kubwa kwa watoto, wazee, waendesha pikipiki, waenda kwa miguu wote na zaidi hakuna Gari lililokuwa na uwezo wa kupita hapo.

Hii ndio tunayoita kurudisha kwa jamii “Community Social Responsibility”, kampuni hii ya Hanspaul imetoa msaada ambao utatoa mchango mkubwa sana kwa jamii na sisi kama Serikali tunafarijika kwa kuona wadau wanaunga mkono jitihada za Serikaili kwa kiwango hiki hili ni jambo la kuigwa na Kampuni nyingine wajifunze katika hili.

Katika uzinduzi wa daraja hili Rc Gambo alitumia fursa hiyo alisikiliza kero za wananchi waliohudhuria na ambao wamelalamikia uuzaji holela wa maeneo ya wazi ya Serikali hali inayopelekea uhaba wa maeneo ya kujenga huduma za kijamii kama zahanati na shule huduma ambazo hazipatikani katika kata ya Engutoto hiyo hivyo wameiomba serikali itatue tatizo hilo ili wananchi wapate huduma bora za ijamii.

Akiwasilisha kero zake mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bi. Zaituni Marunda amesema kuwa licha ya uuzaji holela wa ardhi kuna migogoro ya ardhi katika kata hiyo na wananchi wengi wanaomiliki ardhi bado hajapatiwa hati jambo ambalo linawapa wasiwasi kuwa huenda ardhi zao zikamegwa na wawekezaji.

Aidha Neema John aliongeza kuwa kwa kipindi kirefu katika maeneo hayo wamekuwa wakisumbuliwa na kero za maji, umeme na Zahanati hivyo wameiomba Serikali iwasaidie kutatua kero hizo znazowaathiri zaidi kinamama ambao hutembea umbali mrefu wakitafuta huduma za maji pamoja na kupata taabu wakati wa kujifungua.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ameagiza ofisi ya Mkurugenzi kumkabidhi ripoti ya maeneo ya wazi ya jiji yaliyouzwa kienyeji ili aweze kushughulikia kero na pia aliweza kuhamasisha ujenzi wa Zahanati ya Kata kwa kuchangia Bati 100 na kuungwa mkono na Bw. Hans Paul aliyetoa matofali 5000 huku Bw. Jagjit Aggarwal akichangia mifuko ya saruji 200 na Mkurugenzi wa Jiji Bw. Athumani Kihamia kuahudi kukamilisha ujenzi wa zahanati hiyo.

Daraja la Mto kijenge lilioanza kujengwa mwezi Juni na kukamilika Agost 2016 lina upana wa Mita 20, uwezo wa kupitisha magari yenye uzito wa Tani tatu(3), urefu kwenda juu ni mita 2.2, uimara wa pekee na linaweza kudumu kwa miaka 50; Ujenzi wake umegharimu kiasi cha shilingi milioni 67 .

Comments