Monday, November 21, 2016

RC PAUL MAKONDA AENDELEA NA ZIARA YAKE YA KUIJENGA DAR MPYA KWA KUTATUA KERO ZA WANANCHI

Msafara wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ukiwa eneo la Kisarawe II.
15
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe: Paul Makonda akisalimiana na Mkurugenzi wa Kiwanda cha maji na maziwa (MILKCOM), Said Nahdi (mwenye kanzu), alipotembele kukagua shughuli za kiwanda hicho wakati wa ziara yake.
16
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe: Paul Makonda (katikati), akiwa amefuatana na Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa, na   Mkurugenzi wa Kiwanda cha maji na maziwa (MILKCOM), Said Nahdi  (mwenye kanzu) wakiwa ndani ya kiwanda hicho wakikagua shughuli za kiwanda hicho.
17
Mkurugenzi wa Kiwanda cha Maziwa na Maji (MILKCOM), Yusuph  Said akizungumza na waandishi wa habari wakati wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe: Paul Makonda alipotembelea kukagua kiwanda.
18
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe: Paul Makonda akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa shule ya msingi Tunduwi Songani.
19
Wananchi wa Tunduwi Songani wakishuhudia uwekaji jiwe la msingi la ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa shule ya msingi .
20
Wanafunzi wa shule ya msingi Tunduwi Songani.
21
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe: Paul Makonda  akimsikiliza Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Bakari Mbwana kuhusiana na kero wanazozipata zalugha chafu wanapokwenda katika zahanati .

MKUU wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amesema Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Bakari Mbwana hawezi kupandishwa cheo kuwa Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo mpaka hapo atakapotatua changamoto za zahanati ya Tundu Songani Kata ya Pemba Mnazi.

Makonda aliyasema hayo mwisho wa  ziara yake ya siku ya pili Wilayani Kigamboni Novemba 20, 2016 wakati alipokwenda kuzindua madarasa ya Shule ya Msingi Tundu Songani,ambapo  mara baada kuzindua madarasa hayo aliongea na wananchi na kusikiliza kero.

“Kwa mamlaka uliopewa na Rais wewe ndio mwakilishi wake katika upande wa afya wilaya ya Kigamboni  uwezi kupandisha cheo kuwa Mganga wa Wilaya hii mpaka hapo utakaponiakikishia kupeleka gari la wagonjwa na kutoa lugha nzuri kwa wateja”alisema Makonda.

Makonda alisema awezi kumtumbua jipu Mganga huyo kwa kuwa ameteuliwa muda mfupi mpaka sasa ana mwezi mmoja  hivyo amempa muda kwa ajili ya kumwangalia katika utendaji wake kama kaimu Mganga mkuu wa Wilaya hiyo.

Hatua hiyo ya Makonda kutoa agizo la kumchunguza Mganga huyo linafuatia wananchi wa Tundu Songani kulalamika mbele ya Serikali ya Mkoa  kuwa mganga huyo ajawai kufika eneo hilo na wananchi kupewa lugha chafu wanapokwenda katika zahanati .

Kwa upande wake Kaimu Mganga Mkuu huyo,alipoulizwa kuhusiana na malalamiko ya wananchi alisema  yeye kama mganga mkuu anachofahamu changamoto iliyokuwepo katika zahanati hiyo gari la wagonjwa akuna.
Naye Mwananchi Asha Abadalah alisema mwanamke Mjamzito akienda katika kituo hicho anambiwa aende katika hospitali ya Wilaya ya Temeke  na Mgaga huyo ajawai kufika katika Kata hiyo ya Pemba Mnazi ni mara yake ya kwanza.

Wakati huohuo katika kusogeza huduma za jamii kwa wanachi Makonda alisema kuhusu kusogeza huduma ya umeme kwa wananchi mradi wa umeme vijijini utawafikia kila mwananchi atapata umeme huo kwa gharama y ash,27,000 na kila mmoja atavuta.Alisema utaratibu wa kupata fomu watatangaziwa wote na Watendaji wao wa Mitaa husika
Hivyo wananchi wawe wavumilivu kwa muda wasubilie mradi huo ufike ili wote waweze kupata umeme wa bei raisi .
22
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe: Paul Makonda akisikiliza kero za wanachi katika mkutano wa hadhara ulifanyika katika uwanja wa shule ya msingi Buyuni ikiwa mwisho wa ziara siku ya pili katika Wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam.
23
Mkazi wa Buyuni akielezea kero zake.
24 25
Wananchi wa Buyuni wakiwa katika mkutano wa hadhara.
1
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe: Paul Makonda (katikati) akisaini kitabu cha wageni alipotembelea daraja la Nyerere lililopo Wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam wakati wa ziara yake ya kuangalia na kutatua changamoto za wananchi ikiwa ni mwisho wa ziara siku ya pili kwenye Wilaya hiyo (kulia), Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Profesa Godius Kahyrara, Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa.
PICHA ZOTE NA PHILEMON SOLOMON-FULLSHANGWEBLOG
01
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa akimuelezea Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kuhusiana na tozo  ya magari  kuvuka katika daraja la Nyerere wilayani.
  
 Mgandilwa, amelitaka Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kuangalia upya  tozo  ya magari  kuvuka katika daraja la Nyerere wilayani humo  ikiwa ni pamija  na kutaka magari yote ya  serikali na watumishi wa umma wanaofanya kazi katika halmshauri hiyo kutokulipa tozo hiyo.
Mkuu huyo wa wilaya alitoa kilio hicho  mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul akonda, wakati wa ziara  ya mkuu huyo wa mkoa ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi  mkoani humo.

Mgandilwa alisema, kitendo cha  magari  ya halmshauri hiyo na watumishi wa umma wanaoishi nje ya halmshauri kutozwa fedha kuvuka katika daraja hilo   kinaleta changamoto kubwa  na kukwamisha ufanisi.
Alimuomba Makonda kuingilia kati suala la gharama hizo  na kuitaka NSSF kuziondoa kwa magari yote ya halmshauri na  watumishi.

“Kila gari  ya halmashari inayopita katika daraja hili inatozwa fedha. Hasa ikizingatiwa kuwa halmashauri hii ni mpya hivyo  watumishi wengi wanatokea nje  ya halmashauri,”alisema Mgandilwa.

Alielezea changamoto nyingine kuwa ni  kipande cha Kilometa 1.5  cha barabara ya vumbi kutoka katika daraja  hilo upande wa Kigamboni.
“Hii barabara licha ya kutumiwa na magari mengi  yanayopita katika daraja hili, lakini  haijajengwa kwa kiwango cha lami hivyo wananchi kupata kero kubwa   kutokana na vumbi ,”alisema Mgandilwa.
2
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Profesa Godius Kahyrara  akitoa ufafanuzi kuhusu suala la tozo la daraja daraja la Nyerere lililopo Wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Akitoa ufafanuzi kuhusu suala  la tozo  ya daraja hilo, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Profesa  Godius Kahyrara, alikiri kupokea malalamiko ya watu wengi kutaka kupunguziwa au kuondolewa tozo hiyo.
“Ni kweli tumekuwa tukipokea malalamiko hayo kutoka kwa wananchi mbalimbali, lakini suala ni kwamba sisi kama NSSF huwa hatupangi viwango vya tozo za kuvuka daraja bali tunapokea maelekezo kutoka  wizara husika (Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi),”alisema Profesa Kahyaraa.
Alisema atawasilisha suala hilo katika wizara  husika ili kuona uwezekano  wa kuondoa tozo hiyo ama kupunguza.
Mbali na hayo, Profesa Kahyarara, alitaja changamoto zingine kuwa ni  vijana kuligeuza daraja hiyo kuwa kijiwe na wengine kuwa na nia ovu ya kulihujumu kwa kuharibu miundombinu, ingawa ulinzi umeendelea kuimarishwa.
3
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akifafanua.
Kwa upande wa Makonda, alisema, suala la tozo ya magari ya halmashauri na watumishi  kuvuka katika daraja hilo atazungumza na waziri mwenyedhamana.
4
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mhe: Paul Makonda (kushoto), akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa wakielekea kugagua miundombinu ya daraja hilo.
5
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe: Paul Makonda (kushoto), akiangalia mti uliopandwa na  Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa.
6
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe: Paul Makonda akiwa na kamati ya ulinzi na usalama pamoja na viongozi wengine wakiangali mtaro wa wakupitishia maji katika daraja la Nyerere lililopo Wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam.
7
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mhe: Paul Makonda akiwa na kamati ya ulinzi na usalama pamoja na viongozi wengine wakikagua miundombinu ya daraja hilo.
8
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mhe: Paul Makonda akizungumza na wananchi   wanaoshi eneo la daraja Nyerere lililopo Wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam ilipoishia barabara ya kiwango cha lami aliposimama na msafara wake ili kusikiliza kero na changamoto wanazozipata katika eneo hilo.
Akihutubia wananchi wanaoishi jirani na daraja hilo,Makonda alisema, tayari mkandarasi wa ujenzi  wa kipande cha barabara cha kilometa 1.5 inayounganisha daraja la Nyerere  atanza kujenga kipande hicho kwa kiwango cha lami.
“Mkandarasi aliyejenga daraja  hili ndiyo ataendelea na ujenzi  wa kipande  hiki kilichobakia.Pesa zipo na ndani ya wiki mbili kuanzia sasa  ujenzi utaanza,”alisema.
9
Wananchi wanaoishi karibu na mradi wa daraja hilo wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mhe:   Paul Makonda (hayupo pichani) alipo simama na msafara wake.
10
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe: Paul Makonda akisikiliza kero za wananchi aliposimama na msafara wake eneo la Kibada Wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam.
11
Mkazi wa Kibada, Bi Siwazuri Abdalah akimuelezea Makonda kero anazozipata katika Hospital ya kibada.
12
Mkuu wa Idara ya Uifadhi wa Mazingira na Usimamizi wa Taka Ngumu, Fanuel Kibera akimuonyesha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda (katikati), mchoro wa dampo la kisasa  litakalojengwa eneo la Kisarawe II Kigamboni.
13
Muonekano wa eneo litakalojengwa dampo la kisasa  Kisarawe II Kigamboni.
26
Vikosi vya ulinzi na usalama wakisaidia kulisukuma gari la  Clouds Media liliponasa katika mchanga ene la Kisarawe II wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kukagua eneo litakalojengwa dampo la taka la kisasa.

No comments: