Wednesday, November 09, 2016

WANAMGAMBO ZAIDI YA 200 WASHIRIKI ZOEZI LA OPERESHENI KOMAZA MKOANI IRINGA


Wanamgambo zaidi ya mia mbili wameshiriki katika zoezi la oparesheni komaza mkoani Iringa ambalo limezinduliwa Rasmi na mkuu wa Mkoa huo Bi Amina Masenza.

Akizindua zoezi hilo katika viwanja vya shule ya msingi Mlandege mkoani Iringa likiwa limewakusanya vijana toka vijiji vya Mboliboli, Wasa, Idodi na kwingineko wilayani Iringa lengo likiwa ni kuwajengea uwezo Wana-mgambo na kuwaandaa kuwa vijana wazalendo kwa taifa. 

Zoezi hilo ambalo litachukua siku nne porini likihusisha mazoezi ya ukakamavu pamoja na mazoezi mengine ya kijeshi kwa wanamgambo hao, limeandaliwa na kamanda wa mgambo wa wilaya ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richald Kasesela ambaye ameyaomba makampuni ya ulinzi kuanza kuwatumia vijana waliopitia mgambo ili kupunguza idadi ya vijana wasio na ajira mtaani.
Mkuu wa wilaya ya Iringa Akimkaribsha Kamanda wa mgambo mkoa ambaye pia ni mku wa mkoa wa Iringa Bi Amina Masenza.
Mh Richald Kasesela akizungumza na Vijana wa mgambo.

Akimkaribisha Mkuu wa mkoa wa Iringa Mh Kasesela amesema “Tumeamua kuwa na kikosi mahili ili kisaidie kupambana na majangili pamoja na wahamiaji haramu ambao wamekuwa tishio katika wilaya yetu” 

Mafunzo hayo yataenda sanjali na zoezi la kulenga shabaha pamoja na kuweka kambi porini kwa siku nne ambapo Mh Kasesela atashiriki pia.

Katika hotuba yake kwa vijana wa mgambo, Mkuu wa mkoa wa Iringa, Bi Amina Masenza amesisitiza kuwa Jeshi la mgambo lina msaada mkubwa sana katika ulinzi wa taifa hivyo ni muhimu sote tukachukulia mafunzo haya kama chachu ya maendeleo, ulinzi na usalama hivyo amewataka viongozi wote wa siasa waache mara moja kuingilia shughuli yeyote inayohusishwa na jeshi hili la mgambo kwani jeshi halina itikadi yoyote. 

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, mshauri wa mgambo wilaya ya Iringa afande J.M KITA amewashukuru baadhi wa wadau kwa misaada waliyotoa katika kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa. 

Afande KITA amewataja baadhi ya wadau waliochangia kuwa ni pamoja na ndugu Sallim Asas aliyetoa shilingi milioni moja ambayo imeziingizwa moja kwa moja katika kughalamia chakula kwaajili ya vijana hao, naye meneja wa TANROAD wilaya ya Iringa ametoa Mchele kwaajili ya vijana hao. Kisha Afande KITA akatoa rai kwa wadau ambao wataguswa kusaidia maana bado kuna uhitaji wa msaada wa hali na maali ili kufanikisha ziezi hilo.

Katika kuhakikisha zoezi linaenda sawa Bi Amina Masenza Akatoa gunia la mahindi ili likasaidie chakula kwa wanamgambo wakiwa mafunzoni na akatoa shukrani kwa wadau na kusema kuwa sasa kuna uhakikia kuwa vijana hawatapata shida kwenye suala la chakula.
Makamanda wa mgambo wakisikiliza jambo toka kwa muu wa mkoa.

No comments: