RAIS MAGUFULI AWATUNUKU MAOFISA 194 CHEO CHA LUTENI USU

Bendi ya Jeshi la Ulinzi la WananchiV (JWTZ) likiingia uwanjani wakati wa sherehe za kutunuku Maafisa 194 wa Jeshi hilo katika viwanja vya Ikulu leo Jijini Dar es Salaam 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishiriki kuimba wimbo wa Taifa wakati wa sherehe za kutunuku kamisheni Maafisa 194 wa Jeshi hilo katika viwanja vya Ikulu leo Jijini Dar es Salaam 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua gwaride wakati wa sherehe za kutunuku Maafisa 194 wa Jeshi hilo katika viwanja vya Ikulu leo Jijini Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika mafunzo wakati wa sherehe za kutunuku Maafisa 194 wa Jeshi hilo katika viwanja vya Ikulu leo Jijini Dar es Salaam. 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwatunuku kamisheni Maafisa wapya 194 wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi (JWTZ) 
Maafisa wapya 194 wakila kiapo cha uadilifu baada ya kutunukiwa kamisheni katika viwanja vya Ikulu leo Jijini Dar es Salaam. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimueleza jambo Mkuu wa Chuo cha Maafisa wa Jeshi (TMA) Meja Generali Paul Massao(Kulia) kushoto ni Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange akiongea na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, wakati wa sherehe za kutunuku Maafisa 194 wa Jeshi hilo katika viwanja vya Ikulu leo Jijini Dar es Salaam 
Mkuu wa Chuo cha Maafisa wa Jeshi (TMA) Meja Generali Paul Massao akitoa taarifa fupi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ya mafunzo kwa maafisa wa jeshi ambapo alisema kozi ya mafunzo hiyo ya mafunzo ilianza na wanafunzi 222 kabla ya kuchujwa na kubaki 194 kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kutofikia viwango. 

PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO 

……………………………………………………………….. 
Na Jonas Kamaleki- MAELEZO 
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli leo ametunuku kamisheni maofisa194 wa jeshi Ikulu jijini Da re Salaam. 

Kati ya waliotunikiwa cheo cha luteni usu, 26 ni wanawake na 168 ni wanaume ambapo watatu kati ya wahitumu hao wamepewa tuzo kwa kufanya vizuri zaidi ya wenzao katika mafunzo. Akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa Chuo cha kijeshi Monduli, Meja Jenerali Paul Peter Massao amesema ni ofisa mmoja tu kati ya wote ambaye alisomea Uingereza, waliobaki wamesomea Monduli na ni Watanzania. 

Kwa mujibu wa taratibu za kijeshi, Mtanzania yeyote anayesomea nje ya nchi akihitimu inabidi arudi nchini ili atunukiwe kamisheni na Amiri Jeshi Mkuu. Walianza wanafunzi 224 ambapo waliohitimu ni 194 na wengine hawakuweza kuhitimu kutokana na sababu mbali mbali zikiwemo changamoto za kimafunzo,” alisema Meja Jenerali Massao. 

Tukio hili ni la kihistoria kwani limefanyika Ikulu tofauti na miaka yote iliyopita ambapo Amiri Jeshi Mkuu hutunuku kamisheni katika chuo hicho Monduli tangu chuo hicho kilipohamia huko miaka ya 70. Sherehe hizo zilipambwa na gwaride kutoka kwa maofisa hao na kukolezwa na gwaride la kimya ambalo lilifanyika kwa kwa umahili. 

Waliohitimu leo ni awamu ya 59 tangu chuo hicho kianzishwe zaidi ya miongo minne iliyopita. Chuo cha Kijeshi kilianza mwaka 1969, Kurasini jijini Dar es Salaam kutokana na mahitaji ya mafunzo yanayozingatia maadili ya Kitanzania, na baadae kilihamishiwa Monduli, Arusha mwaka 1976.

Comments