Saturday, November 12, 2016

PROF. NTALIKWA ATEMBELEA MRADI WA KUBORESHA HUDUMA YA UMEME KATIKATI YA JIJI LA DAR

Mkurugenzi Mtendaji wa (TANESCO), Mhandisi Felchesmi Mramba (kulia), akimwongoza Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Prof. Justin Ntalikwa na ujumbe wake kutembelea maeneo mbalimbali katika Kituo cha Ilala, jijini Dar es Salaam, wakati wa ziara yake. 
Mkurugenzi Mtendaji wa (TANESCO), Mhandisi Felchesmi Mramba (kulia) akimweleza jambo Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Prof. Justin Ntalikwa (katikati) na Wataalam alifuatana nao katika ziara hiyo, wakati alipotembeleaMradi wa Kuboresha Huduma ya Umeme katikati ya Jiji la Dar es Salaam. 
Baadhi ya mitambo iliyofungwa katika kituo cha Dar es Salaam City Center.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Prof. Justin Ntalikwa (wa kwanza kulia) akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi Felchesmi Mramba (katikati) wakati alipotembelea Mradi wa Kituo cha Kuboresha Miundombinu ya Umeme cha Ilala, jijini Dar es Saalam. Wa kwanza kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Prof. Justin Ntalikwa (wa pili kulia), akimsikiliza Mtaalam kutoka TANESCO, Gibson Abdallah (wa kwanza kulia) alipokuwa akieleza namna mifumo ya umeme katika Kituo cha Ilala inavyofanya kazi. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa(TANESCO), Mhandisi Felchesmi Mramba anayefuata ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo. Wengine wanaofuatilia ni Wataalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini na TANESCO.
Mafundi wakiendelea na kazi za ujenzi wa miundombinu ya umeme Kusambza umeme katika Kituo cha Ilala jijini Dar Dar es Salaam. 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Prof. Justin Ntalikwa na ujumbe aliofuatana nao, wakisikiliza maelezo ya kuhusu namna kituo cha Kudhibiti Mifumo wa Usambazaji Umeme cha Mikocheni, kinavyofanya kazi.
Kaimu Meneja wa Mradi wa Uboreshaji wa Miundombinu Katikati ya Jiji la Dare s Salaam, Mhandisi Iddy Rashid (katikati) akimweleza Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Prof. Justin Ntalikwa (wa kwanza kulia) na ujumbe aliofuatana nao namna mifumo katika Kituo cha Dar es Salaam City Center inavyofanya kazi.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Prof. Justin Ntalikwa leo amefanya ziara ya kutembelea Miradi mbalimbali ya Kuboresha Miundombinu ya Usambazaji umeme jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuangalia maendeleo ya utekelezaji wa miradi hiyo inayotekelezwa katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

Miongoni mwa miradi aliyoitembelea ni Kituo cha Usambazaji Umeme Ilala kinachojengwa chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Japan (JICA), Mradi wa Kuboresha Huduma ya Umeme Katikati ya Jiji la Dar es Saalam katika Kituo cha Dar es Salaam City Centre na Mradi wa Kituo cha Kudhibiti Mifumo ya Usambazaji umeme, kilichopo eneo la Mikocheni Jijini Dar es Salaam.

Mara baada ya kutembelea miradi hiyo, Prof. Ntalikwa amesema kuwa, kukamilika kwake kutaimarisha miundombinu ya usambazaji umeme Jijini Dar es Saalam na hivyo kuwezesha Jiji la Dar es Salaam kupata umeme wa uhakika.

Akizungumzia kituo cha Kudhibiti Mifumo wa Usambazaji Umeme cha Mikocheni, kilichojengwa na Serikali ya Finland na Tanzania ameeleza kuwa, kituo hicho kimefungwa mashine za kisasa zinazotumia teknolojia za hali ya juu kama zinazotumiwa katika nchi zilizoendelea na hivyo, kukamilika kwake kutawezesha kuondoa tatizo la kukatika kwa umeme jijini Dar es Salaam ikiwemo kubaini kwa haraka na moja kwa moja eneo lolote lenye hitilafu kupitia mitambo hiyo na hivyo kuwezesha tatizo kushughulikiwa kwa haraka.

“ Kwa ujumla nimeridhishwa na kasi ya utekelezaji wa miradi ya kuboresha miundombinu ya umeme inayotekelezwa jijini Dar es Salaam. Mradi wa Kuboresha Huduma ya Umeme Katikati ya Jiji la Dar es Saalam, unatarajiwa kuzinduliwa tarehe 16 Novemba,2016 na Mhe. Rais Dkt.John Magufuli. Kukamilika kwake kutakuwa na manufaa makubwa kwa upatikanaji umeme jijini Dar es Salaam,” ameongeza Prof. Ntalikwa.

No comments: